TAASISI ZA BIASHARA YA FEDHA

TheWiseMan

Member
Joined
Nov 17, 2017
Posts
43
Reaction score
59
Habari za hapa.

Leo nimeona jambo (kwa upande wangu naliona kama kero/ tatizo/ shida/ usumbufu).

Nilikuwa na ujitaji wa Statement ya mpesa, nikaingia online kuona kama naweza ipata nikakosa, ikanilazimu kurudi kwenye app ya mpesa, nikapata mini-statement ambayo kiuhalisia haikidhi mahitaji yangu.

Nikafanya mawasiliano voda kuona kama naweza tumiwa kwa email, nikapata mrejesho kuwa kupata statement inabidi ufike ofisini na kitambulisho chako na pia hakuna soft copy ya statement hapo ofisini bali hard copy.

Nikasema ngoja nifike nipate maelezo zaidi, nikaacha yote nikaelekea vodashop. Kufika nikapata maelekezo yafuatayo.

1. Unapaswa kuwa na kitambulisho chako
2. Utalipia elfu saba (7000)
3. Hakuna soft copy bali hard copy.

Nikaaga nikaondoka.

Sasa hoja zangu zimejikita kwenye hayo maelekezo matatu hapo juu.

1. Tupo katika ulimwengu wa kidijitali na kampuni kama Vodacom imekuwa ikijinasibu kwa kuwa kampuni yenye kuendana na technology. Swala la kukosekana statement (full soft copy statement) kwenye APP si tu udhaifu bali uhalisi wa wazi kuwa Tanzania imejaa fursa zilizowazi ambazo zikipata majawabu si tu hamasa kwa walengwa(wateja) Bali utajiri mkubwa sana kwa wafanyabiashara (wawekezaji)

2. Hii inahusu kulipia elfu saba (7000), yani kiufupi ni kuwa, kampuni kama Vodacom na nyingnezo huchukua taarifa zako na kuja kukuuzia ilihali wewe ni mteja kwao (kwenye hili zipo taasisi nyingi sana, naomba nisizitaje ili kutoenda nje ya mada), kwa wataalam wa programming wataelewa nachomaanisha hapa, hizi ni automated systems, zinajiendesha zenyewe baada ya kutengenezwa, mifumo hii imeshawekwa na inafanya kazi lengwa na kumpa mteja huduma na kuhifadhi taarifa za mteja, swala la kuchaji statement ni sawa na uchaji mtu anapotaka kujua kiasi cha dakika au bando alizonazo. Hizi kiuhalisia ni huduma za bure kabisa kwa maana haziigharimu kampuni ( najua wanachaji kwakua wanatoa karatasi), watakuja na utetezi wa kukuambia tunajaji karatasi na wino.

Jibu lao moja tu. Toeni full soft copy statement, kwa maana technology imekuwa huwezi chukua taarifa zangu afu urudi kuniuzia (huu ni wizi).

Changamoto hii katika upande wa fursa ni swala nyeti sana hasa kwa makampuni shindani ambayo wao wataamua kueka huduma hizi bure kwakuwa haziigharimu kampuni hata thumuni endapo watatoa soft copy statement.

Namba tatu nimeijumuisha na namba mbili.

Asanteni
 
Hakuna kitu huwa nashindwa kuelewa kama hiki,

Hata ukienda benki kuomba bank statement kuna amount unachajiwa ambayo kimsingi mimi na sema ni wizi tu


Achilia mbali benki statement, eti ukiomba mkopo wanakutoza processing fee halafu hela ndefu tu. Sasa ukijiuliza kwanini waliita processing fee na wakati huo huo wakati wa marejesho unatozwa riba ndo utaumia kichwa bure

Ki ufupi hizi taasisi za fedha sheria zake zimekaa kiwizi wizi tu sema ndo hivyo tena dunia haiendi bila hizi taasisi kuwepo na uzuri huwa ni kama zina makubaliaono fulani... yaani kinachofanywa na taasisi X hata taasisi Y inafanya hicho hicho japo nyingine huwa zinamodify kidogo kuficha ila ukifuatilia huwa ndo yale yale tu. Hivyo unavyosema swala la fursa za ushindani hapo hakuna maana ni kama kuna mutual agreement kwa taasisi hizi za kifedha
 
Well said Mkuu.

Nami nilikwisha wahi kukumbana na kadhia kama hii.Hii ilikuwa Tigo miaka kadhaa iliyopita nililipishwa Tsh elfu 6 na ushee kupata hiyo statement.Jana nilitamani kupata nyingine lakini nilivyokumbuka hiyo elfu 6 na kitu nikaamua kutulia.

Inasikitisha kwa kweli, Kampuni kama hizi za mitandao ya simu kutoza gharama za juu na kuweka ukiritimba wa kupata hiyo statement.Hata NMB sasa unaweza kupata online kwa kutumia huduma yao ya ChapChap.Naona kuna baadhi ya Taasisi za Fedha nchini bado zimelala au zimeamua kujitengenezea mrija wa kuingiza pesa.
 
Binafsi naona ni wizi wa mchana kweupe na chakusikitisha zaidi, watanzania wengi hawako sambaba na ulimwengu kuwafanya kujua zama hizi inawezekana wakapata hiyo statement online na wasilipe hata kumi (kwa maana haigharimu chochote kupata softcopy statement).


Unajua ukiangalia kwa undani hili swala la statement maana yake ni taarifa zako binafsi, ambapo wao kupitia mifumo yao (software zao) hukusanya taarifa zako wakati unapokuwa unapata huduma kwao, alafu wanarudi kukuuzia elfu saba.

Yani wanakusanya taarifa zao afu ukizihitaji wanakuuzia, wakati binafsi, Ni wizi wa wazi, haiwezekani ukusanye taarifa zangu(mtej wako) afu bado uniiuzie . Wizi kabisa.
 
Taasisi za fedha huwa zina vyanzo vya mapato,kimojawapo ni hizo ada zinazotozwa...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…