PERECY
Member
- Jan 11, 2012
- 29
- 16
Wapendwa wanaJF,
Suala la Katiba Mpya lilianza kupigiwa kelele zamani na wananchi wapenda ukweli na wenye maono akiwepo Makwaia wa KUHENGA, mwandishi wa Kitabu cha CCM NA MUSTAKABALI WA NCHI YETU, ambapo katika Sura ya 15 ameandika: KATIBA MPYA NDIYO HATMA NJEMA YA NCHI YETU.
Mwandishi hapa amesifia utaratibu wa Rais anapomaliza kipindi chake cha miaka 10, kwa utaratibu wa Katiba anapumzika na hilo limewezekana bila kikwazo kutokea ambapo hakuna Rais mstaafu amebughudhiwa na mwenzake hata kama tetesi za ubadhirifu kuwepo. Hivyo amani hata kama ni kidogo.
Tatizo linaonekana katika Mamlaka aliyopewa Rais ya kuteua viongozi wengi - madaraka yasiyo na vizingiti. Taasisi ya HakiElimu imethubutu kuhoji mengi katika kuboresha elimu na demokrasia (ikiwa ni sehemu ya utawala bora), iwapo ilikuja kuonekana 'inaweka vidole katika macho ya wakubwa'. Bahati mbaya sana Rais amesaini Muswada wa Marekebisho ya katiba kuwa sheria, ambapo tayari imeshalalamikiwa haitakidhi/haitafikia na kupokea maoni ya 'walaji' muhimu wa Katiba hiyo ambao ni wananchi wa kawaida kwa ujumla wao.
Kwa kuwa hata Mwalimu Nyerere aliwahi kusema, "Kwa mamlaka haya niliyo nayo naweza kabisa nikawa dikteta....", na bado ni katika Katiba hii hii.
Napendekeza wanaJF mtoe maoni na mapendekezo zaidi ni namna gani Katiba iumbwe ikiwa na vipengele vyenye kuwezesha uanzishaji wa Mamlaka na Taasisi huru za kusimamia utawala bora nchini. Tunahitaji kupiga hatua ya mbele zaidi, kwani suala la rushwa bado ni tatizo, uteuzi wa wakuu wa wilaya, mikoa, mawaziri, majaji, mwenyekiiti wa Tume ya Uchaguzi, mabalozi, n.k., kwa utaratibu wa sasa - unyongaji wa utawala bora ni dhahiri!
Ni mimi mwanaJF mchanga,
Perecy.