Taasisi za mikopo Mkoani Shinyanga zadaiwa kudhalilisha Walimu wanaoshindwa kumaliza marejesho

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2021
Posts
1,147
Reaction score
2,008
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Sophia Mjema ametoa maagizo kwa Jeshi la Polisi kufuatilia na kuwachukulia hatua taasisi za mikopo zinazodaiwa kuwashikilia baadhi ya walimu katika vituo vyao vya kazi wanaposhindwa kulipa madeni yao.

Kauli hiyo imefuatiwa baada ya tamko la Mwenyekiti wa Chama cha walimu Tanzania Manispaa ya Shinyanga, Meshack Mashigala kudai kila mwaka kumekuwa na matukio ya baadhi ya walimu kukamatwa na wakopeshaji na kisha kufungiwa katika ofisi zao na kuwadhalilisha mbele ya wanafunzi wanaposhindwa kulipa kwa wakati.

“Walimu wangu wanapokopa tu riba inakuwa asilimia 20, wanakabidhi kadi za benki na kutoa namba za siri za benki, wakati wa marejesho wanakuta riba imepanda hadi asilimia 100, hali ambayo hawezi kulipa na anaanza kuishi kama ndege na shuleni anashindwa kuhudhuria vipindi alivyopangiwa kufundisha,” amesema Mwenyekiti.

Ameendelea kusema baadhi ya walimu wamenyang’anywa kadi zao za benki baada ya kukopa fedha katika taasisi hizo ambazo nyingi hazijasajiliwa, na wapo waliokamatwa kazini na kuwekwa katika mahabusu wanazozimiliki ambazo ni kinyume cha sheria.

Kamanda wa Polisi Mkoani Shinyanga, George Kyando amesema baadhi ya walimu wamekuwa wakifika polisi kuomba barua ili waende benki kuomba kadi nyingine kwa madai kadi ya mwanzo imepotea.

Kyando amewataka walimu wanapohitaji mikopo waende katika taasisi zinazotambulika na Serikali ambako kuna viwango vinavyotakiwa kisheria.

Chanzo: Swahili Times
 
Baada ya kifo cha magufuri hizi tasisi zimeanza kufufuka kama uyoga
 
dawa ya deni ni kulipa
 
Washikwe hata matyakko yao hao ndio hutumika kwenye uchaguzi mkuu.
Narudia tena wanyooshwe haswa tena na tena,tumewachoka na uchawa wao.
 
Walimu wengi maisha yao yanatisha na sijui shida ni nni. So ajabu kumuona mwalimu amekuja benki kuchukua mshahara huku kavaa yeboyebo. Ulevi,kuwa na wanawake wengi na kuzaa watoto wengi na mishahara yao midogo unadhani hatima yake nn kama sio aibu? Lakini kwa vile huisaidisa CCM kuiba kura acha yawapate hayo kwa woga wao.
 
BAYPORT riba ni 70%, PLATNUM CREDIT riba ni 65%. Hizi taasisi zimesajiriwa B.O.T na wala hazishikiki. Sijui Mali ya nani.

Ushauri: WAALIMU MKOMBOZI WENU NI NMB, CRDB na BENKI YA POSTA/TPB.
 
  • Thanks
Reactions: MCN
Pi
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Sophia Mjema ametoa maagizo kwa Jeshi la Polisi kufuatilia na kuwachukulia hatua taasisi za mikopo zinazodaiwa kuwashikilia baadhi ya walimu katika vituo vyao vya kazi wanaposhindwa kulipa madeni yao.

Kauli hiyo imefuatiwa baada ya tamko la Mwenyekiti wa Chama cha walimu Tanzania Manispaa ya Shinyanga, Meshack Mashigala kudai kila mwaka kumekuwa na matukio ya baadhi ya walimu kukamatwa na wakopeshaji na kisha kufungiwa katika ofisi zao na kuwadhalilisha mbele ya wanafunzi wanaposhindwa kulipa kwa wakati.

“Walimu wangu wanapokopa tu riba inakuwa asilimia 20, wanakabidhi kadi za benki na kutoa namba za siri za benki, wakati wa marejesho wanakuta riba imepanda hadi asilimia 100, hali ambayo hawezi kulipa na anaanza kuishi kama ndege na shuleni anashindwa kuhudhuria vipindi alivyopangiwa kufundisha,” amesema Mwenyekiti.

Ameendelea kusema baadhi ya walimu wamenyang’anywa kadi zao za benki baada ya kukopa fedha katika taasisi hizo ambazo nyingi hazijasajiliwa, na wapo waliokamatwa kazini na kuwekwa katika mahabusu wanazozimiliki ambazo ni kinyume cha sheria.

Kamanda wa Polisi Mkoani Shinyanga, George Kyando amesema baadhi ya walimu wamekuwa wakifika polisi kuomba barua ili waende benki kuomba kadi nyingine kwa madai kadi ya mwanzo imepotea.

Kyando amewataka walimu wanapohitaji mikopo waende katika taasisi zinazotambulika na Serikali ambako kuna viwango vinavyotakiwa kisheria.

Chanzo: Swahili Times
Hizo taasisi za mikopo zingetajwa kwa majina ili tuzijue
 
Vp kuhusu TALA jamani....naambiwa wako vzuri
 
Daah waalimu wanateseka ila wengi wanajiendekeza kwenye ulevi
 
Dawa ya Deni ni kulipa,, na sio kukimbilia Police...

Nishauri tu,, Kama unataka maisha ya amani ni bora usikopeshe yeyote.... Bank wanavotaka dhamana ya nyumba huwa wapo timamu sana.

Punda bila viboko, mzigo hauwezi kwenda.
 
Mwl anayetegemegea mshahara tu hana haki ya kunywa pombe wala kufanya uzinzi. Hela yake ni ya kulisha familia tu!

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom