Taasisi za Serikali zakumbushwa kutumia huduma za posta kusafirisha bidhaa na vifurushi kwa usalama

mkiluvya

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2019
Posts
809
Reaction score
729

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Dkt. Zainab Chaula amezikumbusha taasisi za Serikali kutumia huduma za Shirika la Posta Tanzania (TPC) kusafirisha bidhaa, vifurushi na vipeto kwa usalama zaidi.

Dkt. Chaula ameyasema hayo wakati wa kikao cha Menejimenti ya Wizara yake na viongozi wa TPC wakiongozwa na Posta Masta Mkuu wa TPC, Hassan Mwang’ombe kilichofanyika jana kwenye ukumbi wa Wizara hiyo uliopo Mtumba, Mji wa Serikali, Dodoma ambapo Shirika hilo lilifika ofisini hapo kwa lengo la kujitambulisha na kuwasilisha taarifa ya Shirika hilo kwa Dkt. Zainab Chaula, Katibu Mkuu mpya wa Wizara hiyo.

Ameongeza kuwa TPC imefanya kazi kubwa ya kusafirisha sampuli kutoka hospitali mbali mbali nchini kwenda Maabara Kuu ya Serikali wakati wa kipindi cha janga la virusi vya Corona pamoja na kusafirisha nyaraka za mahakama zote nchi nzima, benki, Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, Mifuko ya Hifadhi za Jamii, hisa za kampuni mbali mbali na kutumia usafiri wa ndege kwenda ndani na nje ya Tanzania.

Ameitaka TPC kuunganisha huduma za posta na anwani za makazi na postikodi na simu za mkononi ili kuhudumia wananchi katika kufanikisha azma ya Serikali ya kurahisisha na kufanikisha usambazaji na usafirishaji wa barua, vifurushi, vipeto na bidhaa kwa wananchi.

“Tunataka mwananchi afikishiwe nyanya nyumbani kwake na sio atumie piki piki kuzunguka kwa muda mrefu na kupiga simu bila kufika kwa mteja kwa wakati,” amesisitiza Dkt. Chaula.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…