robinson crusoe
JF-Expert Member
- Oct 22, 2020
- 762
- 1,236
Kinachotokea nchini ni mchanganyiko ni ukosefu wa maarifa toka kwa wahusika wanaotakiwa kufanya hivyo. Kama alivyosema Mganga mkuu wa serikali, kuna watu wanataka kusikia kinachosemwa na viongozi ndo wachukuwe hatua za kujikinga. Bahati mbaya wanaotakiwa kusema hawasemi ukweli.
Masikitiko makubwa ni pamoja na wenye ufahamu wa juu kabisa; taasisi za utafiti na elimu ya juu. Wapo NIMR, wapo UD, wapo SUA, wapo UDOM, wapo MUHAS, n.k. Hizi ni taasisi zilizostahili kusimamia ukweli na maelekezo ya kitaalamu na kitaaluma. Bahati mbaya nyingine hawa watu wanapotosha watu kwa makusudi.
NIMR wanawauzia watu mchanganyiko wa viuongo vya chakula usiokuwa na taarifa za kitaalamu eti ni kinga ya COVID-19. UD nao wamekuja na hadithi hiyo hiyo ya mafuta ya kichupa cha kujifukiza kilichojaa vitu visivyokuwa na taarifa za kitabibu. Wakati huo wataalamu wa vyombo vya udhibiti serikalini wako kimya, wakishuhudia utapeli wa wataalamu. wenye lengo la kibiashara tu.
Hizi ni taasisi zilizostahili kuja na uvumbuzi wa kuwatia kiburi wanasiasa, badala yake wote wanashiriki utapeli, na kupotosha wananchi kwa lengo la kuuza chupa nyingi, huku watu wakiteketea. Mainjinia wako wapi kututengenezea ventilators? Wafamasia wako wapi kuthibitisha dawa hizi au kuzikataa?
Sasa taasisi za serikali zimejaa umbumbumbu! Hatuoni tofauti ya mpiga ramli tapeli na profesa wa chuo kikuu!