Taasisi za Umma Endeleeni Kutoa Huduma kwa Weledi na Uadilifu ili Kutimiza Malengo ya Serikali ya Awamu ya Sita

Taasisi za Umma Endeleeni Kutoa Huduma kwa Weledi na Uadilifu ili Kutimiza Malengo ya Serikali ya Awamu ya Sita

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

NAIBU WAZIRI KIGAHE - TAASISI ZA UMMA ENDELEENI KUTOA HUDUMA KWA WELEDI NA UADILIFU ILI KUTIMIZA MALENGO YA SERIKALI YA AWAMU YA SITA

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe ameziagiza Taasisi za Umma kuendelea kutoa huduma kwa wafanyabiashara kwa weledi na uadilifu ili kutimiza malengo ya Serikali ya Awamu ya Sita katika kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini.

Vile vile amewaagiza Maafisa wa Taasisi zinazohudumia Kituo cha Huduma za Pamoja Mpakani Tunduma (OSBP) kupunguza vikwazo vya kibiashara visivyo vya lazima kwa wafanyabiashara wanaotumia kituo hicho kinachohudumia Nchi sita zikiwemo Zambia, Zimbabwe Congo-DRC, Botswana, Afrika Kusini na Namibia ili kukuza biashara za mpakani na kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na nchi hizo na kuongeza mapato.

Kigahe ameyasema hayo Agosti 9, 2023 wakati wa ziara yake katika Mkoa wa Songwe ambapo alitembelea Ofisi za Mkuu wa Mkoa, Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO), Wakala wa Vipimo (WMA), Shirika la Viwango Tanzania (TBS) pamoja na Kituo cha Huduma za Pamoja Mpakani (OSBP) Tunduma ili kujionea utendaji kazi na kutatua changamoto zilizopo.

Aidha, amezielekeza Taasisi za WMA na SIDO kuhakikisha zinafungua Ofisi katika Mkoa wa Songwe ili kurahisisha utoaji wa huduma wa taarifa, mafunzo, mikopo na matumizi sahihi ya vipimo kwa wajasiliamali wa Mkoa huo ili kukuza biashara zao na kuongeza pato la Taifa.

Awali akiongea na Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe. Dkt Fransis, Kigahe amesema Wizara yake pamoja na Taasisi zake itaendelea kushirikiana na uongozi wa Mkoa huo ili kuhakikisha kuwa Mkoa huo wa Kimkakati unakuwa na mazingira bora ya biashara na uwekezaji.

Aidha Mhe. Kigahe ameielekeza TBS kuhakikisha bidhaa zote zinazoingia nchini ziwe na ubora unaotakiwa kulingana na viwango vinavyokubalika kimataifa bila kuathiri Sheria Kanuni na Taratibu zilizopo katika Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Eneo Huru la Biashara Afrika (AFCFTA) na Jumuiya nyinginezo.

Vilevile ameiagiza WMA kukagua bidhaa zinazoingia nchini kulingana na vipimo vilivyoandikwa kwenye label ili kulinda afya za Watanzania na kuhakikisha bidhaa wanazonunua zinaendana na thamani ya pesa.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-08-11 at 01.13.20.jpeg
    WhatsApp Image 2023-08-11 at 01.13.20.jpeg
    37.4 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2023-08-11 at 01.13.21.jpeg
    WhatsApp Image 2023-08-11 at 01.13.21.jpeg
    41.6 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2023-08-11 at 01.13.21(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-08-11 at 01.13.21(1).jpeg
    37.3 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2023-08-11 at 01.13.22.jpeg
    WhatsApp Image 2023-08-11 at 01.13.22.jpeg
    29.6 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2023-08-11 at 01.13.22.jpeg
    WhatsApp Image 2023-08-11 at 01.13.22.jpeg
    29.6 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2023-08-11 at 01.13.22(2).jpeg
    WhatsApp Image 2023-08-11 at 01.13.22(2).jpeg
    38.5 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-08-11 at 01.13.23.jpeg
    WhatsApp Image 2023-08-11 at 01.13.23.jpeg
    36.1 KB · Views: 2
Back
Top Bottom