anonymousme
New Member
- May 18, 2022
- 1
- 2
Pamoja na tamko la Waziri Mkuu Kusisitiza na Kuonya Taasisi Za UMMA kufanya Manunuzi kwa Kutumia Mfumo wa Mtandao (taneps) kikamilifu ambao una Uwazi Mkubwa.
Uwazi huu unawezesha kupatikana kwa Mzabuni Mwenye Sifa, Pamoja na Kupunguza Mazingira ya Ubabaishaji na Rushwa. Pamoja na hayo, bado mpaka sasa kuna Maafisa Masuhuri wasio Waaminifu ambao hawako tayari kutii agizo hili Muhimu la Waziri Mkuu.
Inasikitisha sana kuona kwamba huu Ubabaishaji umekuja hata Maeneo Nyeti yanayogusa Maisha ya Wananchi Wanyonge Moja Moja, hususani uendeshaji wa Mchakato wa kumpata Mzabuni (Mshitiri) wa kusambaza Dawa, Vifaa Tiba na Vitendanishi Vya Maabara wa Mkoa.
Kumekuwa na Maafisa Masuhuri ambao wanatumia mfumo wa taneps Nusu, Yaani hatua ya Awali (Pre- qualification) inafanywa kwenye Mfumo wa taneps, hatua zinazofuata zinachepushwa na kuanza kuwasiliana na Wazabuni Shindanishwi kwa Simu na Email wakitaka kupelekewa Nyaraka (Hard Copies) na cds Ofisini!
Tunaomba hawa Maafisa Masuhuri wakumbushwe vizuri kuwa nchi ilishaondoka salama huko na linapokuja Suala la Dawa, Vifaa Tiba na Vitendanishi Vya Maabara wanatakiwa kupatikana Watu Wenye Sifa stahiki, ukizingatia Mkataba unakuwa wa Miaka mitatu.
Maafisa Masuhuri wa Rukwa na Lindi wamefanya ukiukwaji wa hizi taratibu, tunaomba Wahusika wawarudishe kwenye Utaratibu ili Haki itendeke na Washitiri Wenye Sifa tu Ndiyo wahudumie wananchi.