Taasisi zenye kuhusika na maswala ya fedha.

Taasisi zenye kuhusika na maswala ya fedha.

TheWiseMan

Member
Joined
Nov 17, 2017
Posts
43
Reaction score
59
Habari za hapa.

Leo nimeona jambo (kwa upande wangu naliona kama kero/ tatizo/ shida/ usumbufu).

Nilikuwa na ujitaji wa Statement ya mpesa, nikaingia online kuona kama naweza ipata nikakosa, ikanilazimu kurudi kwenye app ya mpesa, nikapata mini-statement ambayo kiuhalisia haikidhi mahitaji yangu.

Nikafanya mawasiliano voda kuona kama naweza tumiwa kwa email, nikapata mrejesho kuwa kupata statement inabidi ufike ofisini na kitambulisho chako na pia hakuna soft copy ya statement hapo ofisini bali hard copy.

Nikasema ngoja nifike nipate maelezo zaidi, nikaacha yote nikaelekea vodashop. Kufika nikapata maelekezo yafuatayo.

1. Unapaswa kuwa na kitambulisho chako
2. Utalipia elfu saba (7000)
3. Hakuna soft copy bali hard copy.

Nikaaga nikaondoka.

Sasa hoja zangu zimejikita kwenye hayo maelekezo matatu hapo juu.

1. Tupo katika ulimwengu wa kidijitali na kampuni kama Vodacom imekuwa ikijinasibu kwa kuwa kampuni yenye kuendana na technology. Swala la kukosekana statement (full soft copy statement) kwenye APP si tu udhaifu bali uhalisi wa wazi kuwa Tanzania imejaa fursa zilizowazi ambazo zikipata majawabu si tu hamasa kwa walengwa(wateja) Bali utajiri mkubwa sana kwa wafanyabiashara (wawekezaji)

2. Hii inahusu kulipia elfu saba (7000), yani kiufupi ni kuwa, kampuni kama Vodacom na nyingnezo huchukua taarifa zako na kuja kukuuzia ilihali wewe ni mteja kwao (kwenye hili zipo taasisi nyingi sana, naomba nisizitaje ili kutoenda nje ya mada), kwa wataalam wa programming wataelewa nachomaanisha hapa, hizi ni automated systems, zinajiendesha zenyewe baada ya kutengenezwa, mifumo hii imeshawekwa na inafanya kazi lengwa na kumpa mteja huduma na kuhifadhi taarifa za mteja, swala la kuchaji statement ni sawa na uchaji mtu anapotaka kujua kiasi cha dakika au bando alizonazo. Hizi kiuhalisia ni huduma za bure kabisa kwa maana haziigharimu kampuni ( najua wanachaji kwakua wanatoa karatasi), watakuja na utetezi wa kukuambia tunajaji karatasi na wino.

Jibu lao moja tu. Toeni full soft copy statement, kwa maana technology imekuwa huwezi chukua taarifa zangu afu urudi kuniuzia (huu ni wizi).

Changamoto hii katika upande wa fursa ni swala nyeti sana hasa kwa makampuni shindani ambayo wao wataamua kueka huduma hizi bure kwakuwa haziigharimu kampuni hata thumuni endapo watatoa soft copy statement.

Namba tatu nimeijumuisha na namba mbili.

Asanteni
 
Back
Top Bottom