Taazia: Balozi Abdulkarim Omar Mtiro (Cisco) 1950 – 2017 kutoka gerezani na Temeke hadi duniani

Mungu amuweke mahali pema peponi Sisco Mtiro,pia umesahau kutaja OCTAR PUB opp.na Ubalozi wa Ufaransa.
 
Hakuwa Cisco alikuwa Antony Itatiro JK akamtumbua Itatiro na nafasi ya Itatiro kama mkuu wa itifiki ikachukuliwa na balozi Mohammed Maharage.
 
May all beings attain enlightenment.

Mohamed Said Naona picha nyingine hazionekani.

Umenikumbusha mabitozi wa zamani kina balozi Maharage.

Balozi Maharage alivyokuwa kijana akipita maskani hakosi kuwa na copy ya Newsweek au Time Magazine au kitabu cha James Hadley Chase.

Hawa kaka zetu walituhamasisha sana kufuatilia habari zinazoendelea duniani miaka hiyo ya Nyerere.
 
yap,ndo huyu jamaa alitaka kupiga
 
Nnangale,
Kisa kile ni muhimu sana si kwake tu bali hata kwangu.
Naamini kilimfunza Cisco ukweli wa mambo.

Sikutaka kuingiza machungu katika taazia yake.
ama kweli bro wewe nguli wa haya mambo, swaumu njema.
 
Nnangale ni kidogo tu mie bado mwanafunzi.
 
Al Watan,
Nimerekebisha sasa picha zote zinaonekana vizuri.
Ingia hapa:
Mohamed Said: TAAZIA: BALOZI ABDULKARIM OMAR MTIRO (CISCO) 1950 – 2017 KUTOKA GEREZANI NA TEMEKE HADI DUNIANI
 
Dah Ndesamburo kafariki kabla ya Cisco ila sijaona ukimwandikia haya au hana cha kuandikwa?
 
Pole sana hapa pameondoka Gwiji wa Itifaki
 
Dah Ndesamburo kafariki kabla ya Cisco ila sijaona ukimwandikia haya au hana cha kuandikwa?
Ndesamburo na Saigon havichangamani kama mafuta na maji.

Kwani kwao Ndesamburo hana watu wanaomjua wa kumuenzi?

Mtu hawezi kumuandika tu mtu asiyemjua, hawa vijana wa zamani wa Gerezani/ Mchafukoge/Mwembetogwa/Dar wanajuana ndiyo maana wanazikana.
 
Sodoliki,
Mengi sikueleza kwa kuwa huwezi kuandika kila kitu.
 
Cisco alikuwa mcheshi na aliyekuwa anapenda watu. Nakumbuka pia alikuwa anapenda muziki. Enzi hizo tukiwa Chuo Kikuu DSM tulikuwa tunakwenda kumtembelea pale Chuo cha Diplomasia mimi na Mwandembwa na kusikiliza muziki kwenye 'music system' yake.
Dingswayo,
''...atanikumbuka katika, ‘’whatsapp,’’ kwa kuniwekea ‘’clip,’’ ya Earl Klugh mpiga gitaa wa jazz maarufu ambae sote mimi na yeye tukimpenda kwa miaka au, ''clip,'' ya mpiga jazz yeyote yule. Nami kwa kukataa kushindwa na kutaka kuoneshana mizungu nitamrushia, ''clip,'' ya Wes Montgomery, mpiga gitaa nguli lakini wa enzi kabla ya Earl Klugh.
(Kutoka kwenye taazia niliyomwandikia Cisco...)
 
cisco alikuwa mtu wa watu sana! wakuu wengi wa itifaki mambo ya nje ni watu wanaofanana tabia........... nakukumbuka ulivyokuwa mratibu wa mkutano wa sadc 2003
pumzika kwa amani mzee cisco mtiro
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…