Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
TAAZIA: HAMZA RIJAL MCHEZAJI WA ZAMANI WA MALINDI ANAMKUMBUKA MOHAMED MSOMALI
Mohamed Msomali
(Picha kwa hisani ya Vijana Wapenda Soka wa Kariakoo)
ASALAAM ALAYKUM!
In Lilahi wa Ina Ilahi Rajiuna.
Mohamed Msomali Katutoka
na Hamzah Rijal
Katika mchezaji ambaye namkumbuka kwetu huku Afrika Mashariki mwenye _Quality_ ya Boby Moore wa England na Frantz Backenbeur ni Mohammed Msomali na Kadir Farah.
Msomali akiweza kuzuwia mpira kwenye Box akaanza safari taratibu, mwili wake ulikuwa mwembamba lakini akiweza kucheza rafu usiweza kuamini.
Marehemu Kilambo alikuwa na nguvu na akitisha yeye na Kapera, mara mmoja Yanga na Cosmopolitan, Kilambo kishachafua sawasawa kina Jamil, Aden, Marando, Iddi Balozi ikawa wapo taabani, Msomali akampa fundisho Marehemu Kilambo alichukua mpira kisha akafanya umemponyoka, Kilambo hakujuwa kama ametegewa kwenda kupaua aliekewa kile tunaitwa Kisiki, Kilambo alikuwa mzima akarudi kiwanjani lakini alijua kakutana na mwamba mwenzake.
Bahati mbaya sana Tanzania kuwa na watu kama Msomali, Emil Kondo, Sharifu, Hemed Seif, Khalid Abeid kwa nyakati zile ambao kwa leo wangesaidia sana pale midfield ambayo haina ubunifu.
Msomali akiweza kucheza namba 4 au 6 na mara nyengine akicheza 5. Kwenye Taifa kabla ya Combination ya Omar Zimbwe na Goboss ilikuwa unastaladha pair ya Zimbwe na Msomali.
Mwaka wa 1999 nilikutana na Marehemu Msomali pale Morogoro nikiwa kuna Mkahawa karibu na Stand ya Mabasi, Msomali alikuwepo hapo kenda kula hali yake wakati huo, sikuamini nilipomuona Star ambaye kama nilivyokwisha kutaja alikuwa anaitumikia Taifa na Cosmopolitan haikunifurahisha sana.
Msomali kama Allan Ball kwa umbo lakini akichezesha wenzake na mara nyengine unaweza ukamzungumza kama Johan Cruyff pale anapozuia mpira kisha akatoa pasi akakuambia umrejeshee palepale ambao kazongwa na wapinzani, wakati wake ni yeye na Kadir Farah wa Kenya ndio peke yao wakifanya hivyo, ila Kadir Farah alikuwa na speed, Msomali hakuwa na hio speed.
Cosmopolitan imeondokewa na Taifa Star nayo imeondokewa, Allah amjaalie Janahnatul Firdaws, Ameen.
Kushoto wa kwanza ni Mohamed Msomali akicheza timu ya Kombaini ya East African
Cargo Handling Services katika miaka ya1960/70
Rafiki na ndugu yangu Hamza Rijal ni mchezaji wa zamani wa Malindi Football Club Zanzibar.
Kaniandikia binafsi mistari michache kunieleza habari za Mohamed Msomali lakini nimeona niweke hapa kwa faida ya wasomaji na wapenda soka kwa ujumla.
Kwanza nimecheka nilipokuwa namsoma Hamzah khasa pale alipoeleza staili ya uchezaji wa Msomali katika kupunguza nguvu za wapinzani wake.
Nimecheka kwa saabu yeye Hamza akicheza nyuma na alikuwa ‘’no nonsense player.’’
Alikuwa kama Msomali bingwa wa kuwaadhibu, ‘’strikers.’’
Sasa ungekuwa unamjua Hamza nje ya uwanja kwa ule upole na ustaarabu wake kisha ukamuona uwanjani anavyowaparamia, ‘’strikers,’’ ungejiuliza inakuwaje huyu mtu akawa hivi?
Njiwa nje ya uwanja na tai ndani ya uwanja?
Sijashangaa hata kidogo kwa ''tasnifu,'' hii yake ya Mohamed Msomali kwani Waingereza wana msemo wao, ‘’Birds of a feather fly together.’’
Hamzah Rijal amepata elimu yake ya juu Libya na Scotland. Baba yake marehemu Zubeir Rijal alisoma Chuo Kikuu Cha Oxford katika miaka ya 1940.
Hamzah Rijal