TAAZIA: Komredi Kingunge Ngombale Mwiru (1932 – 2018)

Mohammed said, you are a living history legend in East Africa.

The history of this country should be rewritten.

We need to the TRUE history of TANGANYIKA , and Mohamed said and others should help to rewrite it.
 

We humjui huyo mzee, hayupo huru kama huyo Ngombale anayemzungumzia, yameingia mambo mengi yasiyo na maana yoyote, yaani kamweka Ngombale kama Raisi wa nchi
 
We humjui huyo mzee, hayupo huru kama huyo Ngombale anayemzungumzia, yameingia mambo mengi yasiyo na maana yoyote, yaani kamweka Ngombale kama Raisi wa nchi
Kituko,
Kweli mimi simjui Ngombale Mwiru kumfahamu kwangu ni kupitia
watu ambao sote mimi na Mzee Ngombale tulikuwa karibu nao.

Lakini hapa nimwemwandika Mzee Ngombale kutokana na yale ambayo
kwa kiasi fulani mimi nimeyajua baadhi kwa kushiriki.

Majlis itanifaika kama utatueleza unavyomfahamu Mzee nNombale.
 
Mzee kwanini usikae na Yeriko nyerere umuongezee maarifa, siku ukistaafu kuandika historia tutakosa mambo mazuri
 

Wala sina shida na wewe, nasikitika unavyotumia Kalamu yako vibaya, nasikitika kwa jinsi unavyojaribu kuandika vitu visivyo na uhusiano ili mradi unachokitaka kiwe

Umeandika haya hapo juu
1: "Katika hali kama hii vipi Ngombale Mwiru aliyekuwa mfuasi wa Kanisa Katoliki angeweza kusalimika katika mfumo huu kwani yeye alianza kuonyesha fikra za kupinga dini na kuwepo kwa Mungu mapema sana akiwa mwanafunzi wa darasa la sita",
KAKA HAKUNA HATA KAULI MOJA YA NGOMBALE ALIYOTAMKA KUPINGA UWEPO WA MUNGU, unamlisha maneno marehemu, hujapata kusoma alivyochukizwq na Balozi wa Russia pale Kivukoni aliposema hakuna Mungu?

2: "Ally Sykes ndiye aliyempa Ngombale Mwiru kadi za TANU atafute wanachama"
Hapa ulikiwa unamaanisha nini?, Ngombale hakupewa Kadi za TANU na TANU, kupewa kadi na Ally Skykes unataka kumaanisha kuwa bila Sykes Hizo kadi za TANU zisingegawiwa kwa Ngombale?, Kwa kifupi Ngombale alipewa jukumu la kugawa kadi za TANU na chama sio Mtu

Yapo mengi yanayokera kwenye Taanzia yako kiasi yanamaliza Ladha kwa anayekusoma kwa jicho la tatu
 
Kituko,
Bahati mbaya kuwa unaona mimi natumia kalamu yangu sivyo.

Lakini ukweli uliopo ni kuwa publishers wakubwa duniani kama Oxford University Press,
East Africa na New York, Minerva Press London wamechapa kazi zangu.

Hapa nyumbani Abantu Publication halikadhalika wamenichapa pia ukitoa majarida na
magazeti kadhaa ndani na nje ya nchi wanachapa makala zangu.

Kuhusu suala la Mungu katika maisha ya Komredi Ngombale Mwiru hebu soma fikra
zake hapo chini:

"Yule mmoja nani yule aliyesema…“si kuwa Mungu kamuumba binadamu kwa mfano wake
ila ni kuwa binadamu kamfikiria mungu kwa mawazo yake”…hiyo ilinifanya nielewe alaa
kumbe Miungu imeumbwa na mawazo ya binadamu..!

Saa tuje kwenye historia ya Ally Sykes na kadi za TANU:

''Ally Sykes ndiye aliyechora kadi ya TANU na kuchagua rangi na nembo yake.
Rangi alizochagua zilikuwa, nyeusi kuwakilisha taifa la Kiafrika na kijani ardhi ya Tanganyika.
Mfano wa kadi ya TANU ulitokana na kadi yake ya Tanganyika Legion. Baada ya kumaliza
kuichora ile kadi, aliwaendea Tanganyika Standard Newspapers ili wamchapishie. Kutoka
mfukoni mwake mwenyewe alichapisha kadi 1000 za kwanza na akitumia fedha za TAGSA
alichapisha kadi nyingine 2000. Kadi nambari 1 ilitolewa na Ally Sykes kwa rais wa TANU,
Julius Kambarage Nyerere na Ally aliweka sahihi yake kama afisa aliyeitoa. Ilipendekezwa
kwamba kadi chache za mwanzo lazima zipigwe mnada na fedha zitakazokusanywa zitiwe
kwenye hazina ya chama. Abdulwahid, Ally, Dossa Aziz, Rupia na wengine walipanda dau
kununua kadi hizo. Ally alimshinda kaka yake Abdulwahid kwa bei akapata kadi ya TANU
nambari 2; Abdulwahid alipewa kadi nambari 3; Dossa Aziz kadi nambari 4; Phombeah kadi
nambari 5; Dome Okochi, mmoja wa wale wazalendo kutoka Kenya katika TANU alipata kadi
nambari 6 na Rupia kadi nambari 7. Bibi Titi kadi nambari 16; Iddi Tosiri kadi nambari 25.''

''Mtemvu alimuelezea Ally kwa ufupi juu ya mkutano wao na Nyerere Morogoro mjini na
aliomba apewe mara moja kadi 200 za TANU. Ally aliwaandikia na kuwapa kadi za
uanachama wa TANU, Mtemvu na Tambwe na akamwambia mdogo wake Abbas,
awaalike wote wawili kwenye mkutano wa uzinduzi wa tawi la TANU la Dar es Salaam
ambao ulikuwa ufanyike Jumamosi iliyofuata.''

Soma hapo chini kipande cha mahojiano katika ya Prof. Issa Shivji na Mzee Ngomabe
Mwiru:
Ngombale: Mimi ndiye niliyekuwa kijana zaidi katika Kamati Tendaji Kuu ya TAGSA, kupigania haki za Waafrika. Kwa bahati nzuri, TANU ikaanzishwa 0?/0 7/19 54 na kaka Ali Sykes alikuwa kati ya wale kumi na saba walioanzisha TANU.

Baada ya matangazo kuhusiana na kuanzishwa kwa TANU, tukamwomba kaka Ali aje atueleze. Baada ya wiki, kama Katibu Mkuu wa TAGSA, kaka Ali alikuja kutueleza juu ya TANU. Alikuja na kadi za uanachama na mimi nikajiunga palepale.

Shivji: Na huo ulikuwa mwezi wa?
Ngombale: Mwezi huo huo wa Julai, kama wiki moja baada ya kuuundwa TANU. Nikapewa kadi nyingine 100 za kwenda kutafuta wanachama, na eneo langu likawa ni kule PWD.

Kituko,

Hiyo hapo juu ndiyo historia ya kadi za TANU.

Kuuza kadi za TANU ilikuwa kazi inayohitaji ujasiri mkubwa sana kwani TANU ilianza
kupigwa vita na serikali toka siku ya kwanza.

Ngombale Mwiru kupokea kadi kutoka kwa Ally Sykes kwenda kuziuza kwa wananchi
ilitaka ujasiri mkubwa.

Ama kuhusu TANU...
Hiyo TANU, Abdul na Ally Sykes ilikuwa kitu kimoja.

Mikutano ya siri 1950 - 1954 walipokuja kuasisi TANU ikifanyika nyumbani kwa Abdul,
fedha za kuendesha chama toka enzi za TAA wakitoa wao, kadi za TANU za mwanzo
wamenunua wao.

Hizo habari za Mtemvu hapo juu nimesoma katika file za TANU lakini ziko mikononi mwa
akina Sykes sasa zaidi ya nusu karne.

Baadhi ya Nyaraka za Sykes kuhusu historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika nimewapa
Kavazi la Mwalimu Nyerere:


Moja ya Nyaraza za Sykes katika Kavazi la Mwalimu Nyerere



 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…