Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
MAZIKO YA KAKA YETU NUSURA FARAJ
Kama ingekuwa hakuna mvua labda umati uliojitokeza Makaburi ya Kisutu kumzika kaka yetu Nusura Faraj ungekuwa mara mbili ya watu waliofurika hapo Kisutu.
Miezi michache iliyopita Nusura Faraj alimzika mkewe hapo Kisutu na wana Dar-es-Salaam walikuwa wengi hapo makaburini.
Kaka Nusura kwa kumwangalia siku ile katika maziko ya mkewe nilijua alikuwa mgonjwa na nilipata taarifa kutoka kwa jamaa kuwa kaka yetu alikuwa anaumwa.
Miezi michache iliyopita aliniletea mwaliko wa harusi ya mjukuu wake anaoa na tulipokutana katika walima nilifurahi kwani nilimuona amechangamka sana na alinipokea kwa bashasha kubwa.
Nilimshangaza kaka Nusura siku nilipomwambia kuwa mimi nimemjulia Moshi labda mwaka 1961 au 1962 wakati akisoma Moshi Trade School akija mtaani kwetu Liwali Street siku za Jumapili kusalimia jamaa zake.
Mimi nilikuwa na umri wa miaka 9 au 10 hivi.
Kaka Nusura kwa wale wasiomfahamu ni mdogo wake Balozi Abdul Faraj aliyepata kuwa Balozi Ufaransa.
Nusura Faraj ni mtoto wa Dar es Salaam na yeye na ndugu zake waliomtangulia ni Balozi Abdul Faraj na Bi. Masika mstaafu wa Benki Kuu wote ni wanamji na watu maarufu.
Baba yao Mzee Faraj alikuwa akifanya kazi Tanganyika Railways katika miaka ile ya 1920s
Huenda si wengi wakalijua hili lakini kaka Nusura Faraj mimi kanisaidia mengi katika kuelewa yaliyokuwa yakipitika ofisi ya TANU, New Street wakati wa kupigania uhuru.
Nyumba yao ilikuwa Mtaa wa Pemba na New Street si mbali na ofisi ya TANU.
Nyumba hii yao ilikuwa jirani na nyumba ya Mwalimu Sakina mmoja wa akina mama waliokuwa mstari wa mbele katika TANU upande wa akina mama.
Nyumba ya akina Nusura haikuwa mbali na Viwanja Vya Mnazi Mmoja ambako mikutano ya TANU ilikuwa ikifanyika.
Kwa ajili hii basi kwa mapenzi yake ya chama cha TANU alikuwa mara nyingi akifika ofisi ya TANU kuwaangalia viongozi mbalimbali ambao majina yao yakivuma katika kupigania uhuru wa Tanganyika.
Nathubutu kusema kuwa kaka Nusura alikuwa kati ya watu wachache waliobakia walioshuhudia harakati za uhuru kutoka New Street katika miaka ya 1950s kwa macho yake mwenyewe.
Nilikuwa nikitatizwa na jambo lolote kaka Nusura ndiye lilikuwa kimbilio langu.
Kaka Nusura kayaona yote kwa macho yake ingawa alikuwa mdogo lakini alikuwa na akili zake kamili.
Kiasi cha miezi miwili iliyopita nilimpigia simu kumuuliza kuhusu Rashid Ali Meli.
Huyu Rashid Ali Meli alikuwa Bwana Fedha wa Dar es Salaam Municipal Council na ni kati ya wanachama wa mwanzo wa TANU waliohudhuria mkutano wa kwanza wa TANU Ukumbi wa Arnautoglo mwezi August 1954 uliohudhuriwa na watu wasiozidi 20.
Rashid Ali Meli alitoa fedha za Dar es Salaam Municipal Council kumpa Iddi Faiz Mafungo atie kwenye safari ya Nyerere UNO 1955.
Alipopokea simu yangu kaka Nusura alinifahamisha kuwa amelazwa Hindu Mandal Hospital.
Sikutaka kumweleza nilichokuwa namtafutia lakini kwa kujua kuwa nina jambo alisisitiza nimweleze.
Nusura alinieleza kuwa akimjua vyema Rashid Ali Meli kijana wa Kingazija na akanitajia hadi jina la mkewe.
Akaniambia kuwa alikuwa akikaa Mtaa wa Pemba na Sikukuu na nyumba yake ikitazama Kariakoo Market lakini hajui alikwenda wapi yeye na mkewe.
Taarifa hii ilinitosha.
Nikamshukuru na tukaagana.
Nimepoteza kaka na moja ya vyanzo vyangu vya historia ya TANU na mji wa Dar es Salaam.
Allah amsamehe dhambi zake na amuweke mahali pema peponi.