mdukuzi
JF-Expert Member
- Jan 4, 2014
- 20,925
- 51,688
Mwaka 1983 Mzee wangu alihamia Tabata,kipindi hicho kikiwa ni kitongoji duni kabisa,maji shida,barabara mbovu ,kumepoa.
Taratibu mpaka mwanzoni mwa miaka ya 2000 Tabata inaanza kuchangamka,tunapata jirani ambaye ni Mzee John Alphonso Nchimbi,nyumba yake inaangaliana na nyumba yetu.
Wazee hawa wanashikana urafiki maana ni age mates,.na wanafariki kwa kupishana miaka mitatu tu.
Mzee wangu akifariki 2019,na Mzee Nchimbi 2022.
Sikuwahi kuota kuwa Emmanuel Nchimbi angekuja kuwa mtu mkubwa,harakati zake za kisiasa kuanzia UVCCM niliona ni kupoteza muda,connection alizokuwa nazo mzee wake,niliamini kwa elimu yake angeingia serikalini angekuwa mbali...
unamkumbuka Dj Rankim Ramadhan,huyu baba yake alikuwa kiongozi enzi za Mwinyi na Mkapa akiitwa Ramadhan Nyamka.
Mimi nilikuwa rafiki wa DJ Rankim ,DJ Rankim alikuwa rafiki wa Emmanuel Nchimbi,watoto wa wakubwa enzi hizo,mimi sikuwahi kuwa karibu na Emmanuel Nchimbi. Sikupenda siasa nilipenda mlengo mwingine wa muziki.
Soma Pia: CCM yamchagua Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza katika Uchaguzi wa Oktoba 2025
Baada ya Dk Emmanuel Nchimbi kupitishwa na mkutano mkuu kuwa mgombea mwenza wa Rais SSH,nilipata taharifa kuwa mtaani kwetu ni kama sherehe
Ombi la wana Tabata kisiwani,ukiwa VP usihamishe hiyo familia hapo Tabata japo ni uswahilini,majirani wanajisikia fahari kwa kijana wao kupata nafanikio makubwa kisiasa