Tabia 10 za wajasiriamali duniani, kwa mujibu wa utafiti wa UNO ambzo unaweza kujifunza, ukafanikiwa

Tabia 10 za wajasiriamali duniani, kwa mujibu wa utafiti wa UNO ambzo unaweza kujifunza, ukafanikiwa

Mikael Aweda

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2010
Posts
2,973
Reaction score
3,904
Umoja wa mataifa (UN) walifanya utafiti kuhusu tabia za watu matajiri duniani kote. Walijiuliza kwa nini kuna watu maskini na watu matajiri ktk kila nchi iwe nchi tajiri kama marekani na Uingereza ama iwe maskini kama Tanzania na Uganda. Utafiti huo ulihusisha dunia nzima kuanzia Afrika, Asia, ulaya, Amerika, Uarabuni nk. Malawi ndo ilihusika kwa nchi zilizo kusini mwa jangwa la sahara. Utafiti huo ulifanyika kwa miaka 5 ukiongozwa na maprofesa wa masomo ya ujasiriamali kutoka chuo kikuu maarufu duniani cha Havard.

Utafiti huo ulikuja na matokeo ambayo yalionesha kuwa matajiri wote duniani wana tabia (Behaviours) 10 zinazofanana bila kujali kama yuko Afrika, Asia au ulaya – wote wana sifa hizo.
Kila tabia (behaviour) chini yake ina sifa au characteristics au competences tatu (3). Kwa hiyo, matajiri wote wana behaviour 10 na wana sifa au competences 30. ( Tafsiri ya Kiswahili inanipa tabu).
Baada ya kukamilika kwa ripoti ya utafiti huu ikawekwa chini ya United Nations Conference on Trade and Development (UNTAD). Moja ya vitengo vya UN. Mkapa alikuwa mjumbe ktk bodi hii siku za nyuma (sijui sasa)

UNTAD walileta mafunzo yao hayo hapa Tz, kama wanavyofanya ktk nchi zingine. Mwaka 2010 mimi nilipata kuhudhuria Mafunzo hayo yakiratibiwa na TPSF kwa wakati huo. Sasa nasikia mara yanaratibiwa na TIC mara SIDO. Bahati mbaya Serikali yetu haijayachukulia mafunzo hayo seriously. Nikiri hapa kwamba mafunzo yale yalibadilisha kabisa mtazamo wangu kuhusu ujasiria mali na biashara kwa ujumla.

Baada ya kuelezea historia hiyo fupi naomba sasa nitaje mmoja ya tabia ya matajiri duniani kote. Pamoja na competence zilizoko chini yake. Ntaleta tabia nyingie mmoja baada ya nyingine kila wiki kadri Mungu atakavyonijalia.

Tabia za watu matajiri.
1) Goal setting. ( kupanga malengo.)
Utafiti ulionesha kwamba matajiri wote bila kujali nchi anayoishi wamepanga malengo kuhusu biashara au ujasiria mali wao. Utafiti uliyanyambulisha characteristics au compenteces 3 chini ya goal setting ambazo ni;

A) kupanga malelngo ambayo yanawapa changamoto kubwa ktk maisha yao.
Malengo hayo yanawapa changamoto kubwa sana ambayo ndo inawakimbiza ktk maisha yao.
Kwa mfano. Tajiri ana malengo ya kila siku yaani akiamka asubuhi ana malengo ya siku. Amepanga atafanya nini saa mbili, saa tatu , saa nne saa tano mpaka jioni. Tujiulize; ni wajasiria mali wangapi wako hivyo?
B) Matajiri wana malengo ya muda mfupi. Hii kuanzia mwaka moja na hadi zaidi ya miaka tatu. Baada ya muda huo anajitathmini. Kwa mfano. Mimi x nitakuwa na dola milioni 10 baada ya miaka 3
C) Matajiri wote wana malengo ya muda mrefu. Hii kuanzia miaka 5 na kundelea.Kwa mfano. Mimi x nitakuwa na dola milioni 50 baada ya miaka 5.
Kwa hiyo, kila siku wanashindana na malengo au mitihani waliyojitungia wenyewe.
Hivyo basi,
Matajiri wote hufanya tathmini ya malengo yao kila jioni au kila baada ya miaka 2 au zaidi (muda mfupi) na hufanya tathmini ya kila baada ya muda mrefu (miaka 5 au zaidi)
Kwa hiyo, kama alipanga kwamba atakuwa na mil 50 baada ya miaka 5. Baada ya muda huo watajitathmini kuona kama amefikia au la. (Kama amefeli kufikia lengo atajifunza kutokana na makosa yake) Kwa hiyo, kwa miaka yote 5 atakuwa anashindana na malengo yake mwenyewe.

Swali, ni je wewe ulikuwa na malengo gani mwaka 2012. Na je una malengo gani kufikia December 2013? Kama huna ina maana huhitaji tathmini yo yote. Mana kama ukiwa na mil 10 asante mungu, ukiwa na mil 30 Alhamudulilahi, kama una mil 1 vivyo hivyo huna cha kulaumu wala kushukuru. Hutakaa ushindwe wala hutashinda kwa sababu hakuna mtihani wa kujipima nao. Hivyo sivyo walivyo walivyo matajiri.

kwa hiyo kwa ufupisho.
Tabia ya kwanza ni kupanga malengo ( Goa setting) chini yake ina vipengele 3 ambavyo ni .
A) Kujipangia malengo ambayo lazima yanawapa changamoto ngumu ktk maisha yao. na mlaengo hayo yako ktk makundi mawili ambayo ni ( B na C)
B) Wana malengo ya muda mfupi mwaka mmoja hadi miaka 3
C) Wana malego ya muda mrefu yaani miaka 5 au zaidi. (Hawana malengo ya muda wa kati)
Je wewe una malengo hata ya siku ya leo? Una malengo gani mpaka December mwaka 2013, Je baada ya miaka 3. Je, miaka 10 ijayo? Hatuzungumzi ndoto za kichwani. Tunazungumza vitu ulivyokwisha kuviandika na kila mara unavisoma. Kuwaza kila mtu anawza, hiyo siyo hoja.

Jambo jema kuhusu utafiti huu ni kwamba tunaweza kujifunza kutoka kwa matajiri hawa na tukafanikiwa hata kama wewe siyo born entrepreneurs unaweza kusogea ukafikia pazuri. Sote tuanze sasa.

Nawasilisha.

Ukiwa na swali unaweza kunipm au kunipigia. No zangu ziko ktk signature yangu.
.
 
Mkuu, kweli kabisa. Failure to plan is a plan to failure.
 
Back
Top Bottom