Tabia hii kwa Wanaume

Tabia hii kwa Wanaume

ram

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2007
Posts
9,326
Reaction score
8,505
Hii tabia inanikera sana, unakuta ni mkaka au mwanaume mnafahamiana pengine mnaishi eneo moja au manafanya kazi sehemu moja au ofisi zenu ziko jirani au vyovyote vile, mnazoeana na mnakuwa marafiki wa kawaida tu, kumbe nyuma ya pazia mkaka ameshakupenda, siku ya siku anajitoa kimasomaso anakuambia kwamba anakupenda na anataka muwe pamoja, unamjibu vizuri tu kwamba haiwezekani na unampa na sababu kwanini hamwezi kuwa pamoja ktk mahusiano, mwingine si ajabu hata mpenzi/mume wako anakuwa anamfahamu kabisa lakini anakwambia anakupenda anahitaji kamapani yako.

Baada ya kumkatalia sasa, unaona mabadiliko kwa mkaka, yale mazoea yaliyokuwepo awali huyaoni tena, hata ukimsalimia haitikii salamu yako, kifupi anakuchukia anakununia, sasa najiuliza kukukataa ndo sababu ya kunichukia na kuninunia? Mbona awali tulikuwa tunaongea vizuri tu iweje baada ya kunitongoza nikakataa unanikasirikia?

Mnanikera...!
 
cha uso kinauma mbaya
Sasa akusalimie tena wa nini wakati alichokuwa anataka hakiwezekani
 
hahahahahah...hii kweli ni nomaaa
unajua hao jamaa ni wale ambao they not true to themselves...ndio maana mie naonaga bora usemaga mapema shida yako sio kujidai unataka urafi tuu kumbe unalako jambo...be strait forward na sema kuwa wataka more than frendship.

pili hi hivi huyo jamaa kununa au kukuchukia ni kutokana na kwamba anaona amepoteza muda mwingi lakini ukweli ni kwamba he is all to blame...angekwambia mapema tuu asingefika huko.
pamoja na hayo lakini kuna tatizo moja...wanawake wengi ukisema from the begining kuwa unamtaka..basi ndio umempeperusha. sasa ndio maana wengi wanaresolt to pretending kutaka frendship
 
  • Thanks
Reactions: ram
Wee mdada ukikutana na mwanaume wa dizaini hiyo basi,ujuwe kuwa huyo mwanaume hajuwi hata kutongoza kwani mwanamke halisi hatongozwi na kukubali kwa siku moja tu.ukiona mwanamke kakukubalia siku hiyo hiyo basi huyo ni changu,yuko after money(biziness zaidi)
 
Hakuwa na shda na "urafki wa kawaida" lkn hata hvyo sio mstaarabu japo pia kukataliwa kunauma.
 
Kibuti kinaboa! Mtu mzima umejikoki uko na njozi kibao kwa binti au mwanamke ushamzoea unaingiza vokali tu unalipuliwa! Aibu tehe tehe tehe...na urafiki uishe tu sitakuwa na raha...na log in
 
  • Thanks
Reactions: ram
hamna faida... Urafiki kati ya mwanamke na mwanaume ulishawai kuona wapi??? We mwenyewe mume wako au mpenzi wako sio rafiki yako..
 
Mimi sijui labda, wewe ulitaka kuendelea kuwa rafiki yake? basi kuna kitu umependa kwake na kama na yeye ataendelea na wewe nawe utakuja kumtongoza.

Kama hujampenda au umempa sababu zako hajakuelewa wa nini huyo tena? Hahahaha unalialia kumpoteza wewe au unakumbuka viofa ofa alivyokuwa anakupa?
 
Mimi na wasi wasi aliyepigwa chauso ni huyu dada, maana imemuuma alizani jamaa atang'ang'ania kidogo ili akubari jamaa akaishia zake moja kwa moja sasa anamlilia. Wengine huwa ni mbinu ya kukufukuza anakutongoiza siku ambayo anajua uko vibaya kimudi ukimkatalia ndo njia ya kutokea hakusalimii tena ng'ooo
 
Hii tabia inanikera sana, unakuta ni mkaka au mwanaume mnafahamiana pengine mnaishi eneo moja au manafanya kazi sehemu moja au ofisi zenu ziko jirani au vyovyote vile, mnazoeana na mnakuwa marafiki wa kawaida tu, kumbe nyuma ya pazia mkaka ameshakupenda, siku ya siku anajitoa kimasomaso anakuambia kwamba anakupenda na anataka muwe pamoja, unamjibu vizuri tu kwamba haiwezekani na unampa na sababu kwanini hamwezi kuwa pamoja ktk mahusiano, mwingine si ajabu hata mpenzi/mume wako anakuwa anamfahamu kabisa lakini anakwambia anakupenda anahitaji kamapani yako. Baada ya kumkatalia sasa, unaona mabadiliko kwa mkaka, yale mazoea yaliyokuwepo awali huyaoni tena, hata ukimsalimia haitikii salamu yako, kifupi anakuchukia anakununia, sasa najiuliza kukukataa ndo sababu ya kunichukia na kuninunia? Mbona awali tulikuwa tunaongea vizuri tu iweje baada ya kunitongoza nikakataa unanikasirikia? Mnanikera........

Kinachokufanya ukereke ni tabia yako mbaya. Mi naona ulikuwa unamtania tu uliposema humtaki, ukitaraji kumkubali kama angesisitiza ndio maana unakereka kwa kutojua hatarudi tena. Otherwise, mtu mkora kama huyo akikununia hupati hasara yoyote
 
We umempa za uso, tupo tofauti ktk kuhimili vibuti hiyo ndio style yake :bolt::bolt::bolt:
 
Hehehehe! Yashanikuta hayo mara nyingi. Akichuna na wewe chuna tu. Kwanza hakupunguzii chochote.
 
kujitoa kimasomaso sio????

na mimi nataka kujitoa kimasokimaso kwa ko leo..lol
 
Back
Top Bottom