ram
JF-Expert Member
- Oct 5, 2007
- 9,326
- 8,505
Hii tabia inanikera sana, unakuta ni mkaka au mwanaume mnafahamiana pengine mnaishi eneo moja au manafanya kazi sehemu moja au ofisi zenu ziko jirani au vyovyote vile, mnazoeana na mnakuwa marafiki wa kawaida tu, kumbe nyuma ya pazia mkaka ameshakupenda, siku ya siku anajitoa kimasomaso anakuambia kwamba anakupenda na anataka muwe pamoja, unamjibu vizuri tu kwamba haiwezekani na unampa na sababu kwanini hamwezi kuwa pamoja ktk mahusiano, mwingine si ajabu hata mpenzi/mume wako anakuwa anamfahamu kabisa lakini anakwambia anakupenda anahitaji kamapani yako.
Baada ya kumkatalia sasa, unaona mabadiliko kwa mkaka, yale mazoea yaliyokuwepo awali huyaoni tena, hata ukimsalimia haitikii salamu yako, kifupi anakuchukia anakununia, sasa najiuliza kukukataa ndo sababu ya kunichukia na kuninunia? Mbona awali tulikuwa tunaongea vizuri tu iweje baada ya kunitongoza nikakataa unanikasirikia?
Mnanikera...!