Winner Magele
Member
- Jan 9, 2013
- 86
- 49
Mkuu Jacobus, kwanza pole kwa hayo yaliyotokea.Jumamosi tarehe 26/01/2013 nikiwa ofisini mida ya saa mbili usiku mie na jamaa zangu tukisubiri kusikiliza taarifa ya habari (StarTv) jamaa yetu mmoja akingia na watu watatu (mwanamke mmoja) wakiwa na laptops na video camera na kuanza kutafuta switchsockets ili kucharge.
Mwanamke akaenda moja kwa moja kwenye tv na kuizima na kuchomeka charger ya kilaptop chake na kutuacha wenyeji tukiduwaa na hatua hiyo.
Kwa kweli ilituuma mno na sikuvumilia, nikamuomba atafute pengine kwani switchsockets zipo nyingi cha ajabu mdada akasema sisi ndo tutafute pahala pengine pa kuangalia/kusikiliza taarifa hiyo ya habari. Sikuvumilia na niliamka kwenda toa charger yake na kuwasha tv. Baadae mmoja wao akaniambia yule mdada ni Ufoo Saro wa ITV, tulishangaa sana kwa tabia hiyo na kujiuliza mbona busara hana au kwa kuwa ni mwandishi wa habari (tena ITV) au katoka Mzizima (Dar) na kutudharau wa mikoani?
Sasa kama mtu ambae hana simile si angemzaba kibao?
Asiyejuwa MAANA usimwambie MAANA.
Mkuu Jacobus, kwanza pole kwa hayo yaliyotokea.
Kwa sisi tunaomjua Ufoo Sara, ni mwanadada wa shoka kweli kweli na yuko poa sana!.
Kwa hayo uliyoelese, naomba nikuombe samahani kabla kwa sababu siamini kama ni kweli kilichotokea ni hiki ulichoeleza.
Haiwezekani mtu aje na kujichomolea tuu tv, kuna jambo behind ambalo wewe ama ulilisikia na hukulieleza kwa makusudi ama hukulijua kuwa lilitokea kabla na hali lazima ilikuwa hivi
Pasco.
- Lazima huyo dada aliwaona wahusika kabla na kuomba idhini ya kucharge laptop yake!.
- Alielekezwa hapo ilipo tv ndio the only swich socket inayofanya kazi na kuruhusiwa kwenda kuchomoa TV.
- Kwa vile lengo lilikuwa kuwahisha story kwa kuripoti live kwenye habari, due to pressure, alighafilika na kusahau kuwaomba radhi nyinyi mliokuwepo, kughafilika ni ubinaadamu pia!.
- Huyu ndie mwandishi aliyezunguka nchi nzima ndani ya helcopter ya Mbowe ile 2010 wakati mwenzake Makunga alizunguka na CCM! nadhali malipo ya Ufoo Saro baada ya kuwafanyia Chadema very positive reporting unayajua!. na ya Makunga pia unayajua!.
- Nakubaliana na wewe, wako watangazaji wa TV wanaojisikia sana na kujiona wao ni ma celeb, lakini wako watangazaji wengine tuu tena ni wazuri ila hawajisikii kabisa na kujihesabu wao ni watumishi wa watu!. Ofoo Saro, yuu mmoja wa Watangazaji hao!.
Nimeisha sema ofisi yangu haihusiani na masuala ya habari. Aliyewaleta ni mfanyakazi mwenzetu kuja ku'charge' vitendea kazi zao na walikuwa watatu, yeye wa ITV, wa Startv na Uhuru.Nahisi huyu mtuma taarifa ndio atakuwa na makosa. anasema ufoo saro alikuja na mfanyakazi mwenzake. hatujui ofisi hiyo inashughulika na nini. pengine ni sehemu ya majukumu yaliyokuwa yamemleta ufo saro. story iliyoko nyuma ya pazia inaweza kuwa inampa nafasi ya Ufo saro kufanya hivyo.
Jumamosi tarehe 26/01/2013 nikiwa ofisini mida ya saa mbili usiku mie na jamaa zangu tukisubiri kusikiliza taarifa ya habari (StarTv) jamaa yetu mmoja akingia na watu watatu (mwanamke mmoja) wakiwa na laptops na video camera na kuanza kutafuta switchsockets ili kucharge.
Mwanamke akaenda moja kwa moja kwenye tv na kuizima na kuchomeka charger ya kilaptop chake na kutuacha wenyeji tukiduwaa na hatua hiyo.
Kwa kweli ilituuma mno na sikuvumilia, nikamuomba atafute pengine kwani switchsockets zipo nyingi cha ajabu mdada akasema sisi ndo tutafute pahala pengine pa kuangalia/kusikiliza taarifa hiyo ya habari. Sikuvumilia na niliamka kwenda toa charger yake na kuwasha tv. Baadae mmoja wao akaniambia yule mdada ni Ufoo Saro wa ITV, tulishangaa sana kwa tabia hiyo na kujiuliza mbona busara hana au kwa kuwa ni mwandishi wa habari (tena ITV) au katoka Mzizima (Dar) na kutudharau wa mikoani?
Sasa kama mtu ambae hana simile si angemzaba kibao?
Upo sahihi, mtu yeyote anaweza kuwa mstaarabu kulingana na sehemu alipo, watu gani waliopo n.k.. Wakati wakiingia hakukuwa na utambuzi lakini baada ya tukio mwandishi mwenzie alifahamisha kuwa ni Ufoo Saro huyo wa ITV. Nimeweka humo ili kama yupo akanushe na ajisahihishe kutokana na maoni ya wanaJF.Mbona wengine mnamhukumu kabla hamjasikia upande wa pili? Dada huyu mimi ninavyomfahamu ni mstaarabu sana nashindwa kulikoni hata ikawa hivyo? ninashaka na uzi huu huenda kunatatizo lingine na siyo hili.