Tabia hii ya Ufoo Saro wa ITV ni uandishi wa habari au nini!

Status
Not open for further replies.
Huyu Dada yumo humuhumu JF na hana haja ya kukujibu kwa kuwa kuna kilichojificha zaidi hiz tuhuma unazompa kwani ulivyoichomoa Laptop yake ilijaa na akaondoka bila kuaga.
Hata sisi tulishangaa mno baada ya kuelezwa ni yeye na aliondoka bila kuaga baada ya laptop yake kujaa.

Japo alituudhi tulimsema lakini bado akawa mbishi nadipo nilipochukuwa hatua ya kutoa charger yake kwenye switchsocket.

Nimeisha sema ofisi yangu haihusiani na masuala ya habari. Aliyewaleta ni mfanyakazi mwenzetu kuja ku'charge' vitendea kazi zao na walikuwa watatu, yeye wa ITV, wa Startv na Uhuru.
Ofisi yako ina Computer au Laptop ambazo ndio umeandikia thread hii, sasa siamini km bado kuna mahali mnaweza angalia TV moja watu wote na umesema s/socket zimejaa, kwanini huyo aliyewaleta na wewe mwenyeji msimtafutie mgeni socket ingine, km sio mzoefu akajaza na kuondoka zake

Ndiye yeye haswa na hata baada ya ku'charge' ka-laptop kake hakuaga.

Mimi naona kuna kitu kingine huyu Dada kakukosea hadi kumleta humu JF na ninaona umemuelewa ndivyo sivyo katika waandishi wa Habari yeye ni No. 1 na thread yake imo humuhumu mwache akafanye kazi nyingine lkn kukujibu kuhusu socket wakati Laptop ilijaaa nahakika wako wanaume wengine na hata waliomleta walimsaidia
fuatilia hiyo mojawapo ya Post nyingi za kumpongeza ufoo Saro

https://www.jamiiforums.com/tanzani...shi-wa-itv-aliyeko-na-msafara-wa-dr-slaa.html
https://www.jamiiforums.com/habari-na-hoja-mchanganyiko/178304-mtizameni-ufoo-saro-sasa.html

Mkuu Jacobus Nawapongeza sana kwa kujizuia kumpiga makofi huyo dada,naona busara ilitumika zaidi vinginevyo angekutana na vichwa vibovu angesimulia.Huwezi kukuta watu wanaangalia Tv unazima hata kama ni watoto wako neno samahani lazima litangulie.
 
Mikoani bado hii mambo ya king'amuzi na kuzimwa kwa dijitali haijashika hatamu...
Kumbuka wakati TV (nyumba za sinema) zinaanzishwa hapa nchini serikali ilitoa upendeleo kwa mikoa mitano tu licha ya mzee Mengi kulalamika, mikoa iliyobaki iliamua kuanzisha cable TV na watu binafsi kuwa na madishi hivo nyie mliozowea bure poleni.
 
Sawia, kilichonisukuma kuwataarifu wanaJF ni kuwa yeye ni mwandishi wa habari na chombo anachofanyia kazi kinaheshimika mno (ITV).
 
nahisi uzee unanijia!unless mtu aniambie kuwa kuchomoa switch sijui nini kunaweza kufanya mtu aanzishiwe thread?lol!
 
Sawia, kilichonisukuma kuwataarifu wanaJF ni kuwa yeye ni mwandishi wa habari na chombo anachofanyia kazi kinaheshimika mno (ITV).

yatosha kweli?
ni ITV WALIMTUMA?
ni TAALUMA YAKE YA UANDISHI WA HABARI ILIMUELEKEZA KUFANYA HAYA?
sina mamlaka ya kuhoji utashi wako katika hili ila ni maswali tu najiuliza mwenyewe!
 
Sijakataa kuwa ni mchapakazi na sie tulimshangaa kwa kitendo alichofanya na ndio kilichonipelekea kuwafahamisha wenzangu wanaJF kwani ni mwandishi na ni wa ITV. Nilipoichomoa charger yake alichomeka pengine humohumo ofisini.
 
yatosha kweli?
ni ITV WALIMTUMA?
ni TAALUMA YAKE YA UANDISHI WA HABARI ILIMUELEKEZA KUFANYA HAYA?
sina mamlaka ya kuhoji utashi wako katika hili ila ni maswali tu najiuliza mwenyewe!
HAIBA kwa fani na chombo licha ya yeye binafsi.
 
Poleni kwa masahibu hayo ila naamini amejifunza, mtu ni utu siyo utukutu
 
Sijakataa kuwa ni mchapakazi na sie tulimshangaa kwa kitendo alichofanya na ndio kilichonipelekea kuwafahamisha wenzangu wanaJF kwani ni mwandishi na ni wa ITV. Nilipoichomoa charger yake alichomeka pengine humohumo ofisini.

Nimesoma habari yako naona una chuki binafsi na Ufoo si bure"
 
Nimesoma habari yako naona una chuki binafsi na Ufoo si bure"
Tokea lini? Tulikuwa hatukumtambua kabla ya kufahamishwa na mwandishi mwenziwe baada ya kitendo hicho.
 
Labda anadhani yeye ni celebrity na anaamini kuwa celebrity maana yake ni kufanya atakavyo...

Celebrity my butt!!! Mishauo tuu kujifanya OVER BUSY na kazi zao ndiyo MUHIMU KULIKO CHOCHOTE MUDA HUO ...Wana mikogo hawa jamaa zetu wa media ukikutana nao (wengi tuu) huko mikoani wakiwa wametokea DAR ES SALAAM!!!!
 
Ndiye yeye haswa na hata baada ya ku'charge' ka-laptop kake hakuaga.
Japo alituudhi tulimsema lakini bado akawa mbishi na ndipo nilipochukuwa hatua ya kutoa charger yake kwenye switchsocket. Wewe ulitaka tumfanyeje?
Umejijia na kujiingilia ofisi ya watu, na kujichomolea tv na kujichajia laptop yake!. Wewe ulimuuliza huyo mwenzako aliyewaleta?.
 
Umejijia na kujiingilia ofisi ya watu, na kujichomolea tv na kujichajia laptop yake!. Wewe ulimuuliza huyo mwenzako aliyewaleta?.
Hata huyo aliyewaleta alishikwa na butwaa kwa kumuona mdada akichomoa waya wa TV na kuchomeka charger yake ya laptop.
Na nasisitiza kuwa sikuwa na maana ya kumjadili Ufoo Saro binafsi ila kilichompelekea kufanya hivo je ni kwa kuwa MWANDISHI?, tena wa ITV?. Hapo ndio kusudio haswa.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…