Tabia hizi za wageni zinakera

KIMIYAKIMIYA

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2014
Posts
244
Reaction score
321
Hakuna mtu ambaye hajawahi kuwa mgeni na kama bado lazima siku moja utakuwa ugenini, kuna vijitabia ambavyo vinaweza kuwa kero kwa wenyeji wako bila ya wewe kujua.

Binafsi sipendi mgeni anayenitembelea ana simu lakini hana chaja, hivyo ratiba ya kuchaji simu yake inaingiliana na mimi mwenyeji huku akitoa visababu visivyoeleweka vya kwanini hana chaja.

Hebu turushie vitabia vya wageni vinavyokera ili tujirekebishe tukiwa ugenini.

Uzi huo leta sindano tuwashone

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani mgeni wako kuomba chaja tu unakimbilia JF asubuhi hii kuanzisha uzi!
Nadhani wewe binafsi una matatizo makubwa zaidi ya huyu mgeni wako unayemlalamikia.

Si ajabu unahesabu hata kila tonge la ugali analopeleka kinywani mwake. Vitu vingine ambavyo ni trivial potezea brother!
 
Chini kasema "uzi huo leta sindano tuwashone"kazi kweli kweli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mjadala wa kipuuzi kabisa huu
 
Ndio maana siku hizi watu hawatembeleani mnaongelea bar kila mtu anaenda kwakeπŸ˜‚πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…