Tabia ya ' kidada' kwa wadada wa iringa ina tija ktk mapenzi..!?

MORIA

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2011
Posts
706
Reaction score
278
'Kidada' kwa kihehe ni tabia ya kususa...nilimuuliza rafiki yangu wa huko ira akaniambia ni katabia flan kanakoendekezwa kwa sana na wadada wa huko...huyu rafiki akahitimisha ukikijulia hicho 'kidada' basi dada wa kihehe yu tayari kufwariki kwa ajili yako...tulikuwa na wachagga na mambo yao..sasa nawaombeni tukijadili hiki 'kidada' cha wadada wa iringa..je kipo..kina tija? au huyu rafiki yangu ni mzushi tuu..
 

mdau ebu weka topic sawa "kidada" unamaanisha nini?
 
Lazima ujue maana ya hilo neno "Kidada"
Hiyo ni silika iliyo rithiwa toka kwa mtemi Mkwawa kiboko ya Zelewsk!

Kidada ni tokeo la kutokukubali kupelekwa mputa/kuburuzwa/kulazimishwa kwa aina yoyote ile na hutendwa na jamii ya wahehe hasa wanaojitambua!

Mtemi Mkwawa alifanya hivyo nae alirithi toka kwa baba yake Mnyigumba wa pale Rungemba!

Chifu Adamu Sapi alimfanyia hivyo Nyerere pale alipo mpokonya uspika na kumpa waziri wa mali asili!
 
mtemi mkwawa alikuwa na kidada au alikuwa jasiri...kidada si kususa au...asante mkuu
 
Kidada ni Kiburi bana. Kweli wa dada wa Iringa si mchezo kwa KIDADA beee!! Utasikia nyelaa ndi mnyamumooo, ndi mnyabaha yaani mie wa hapa hapa tuuu hahahaha watani zangu hawa bana si mchezo! enzi za mwalim ilikuwa mpaka upate game kwa mtoto wa kihehe unasota mbayaaaaaaaaaa sijui miaka hii utandawazi umewaharibu ndo maana hata NGOMA inaongoza huko kwao!!
 
Duh..kumbe ni kiburi...rafiki yangu aliniambia kuwa hiyo kidada ina faida kwani hapo bint anahitaji kubembelezwa
 
mtemi mkwawa alikuwa na kidada au alikuwa jasiri...kidada si kususa au...asante mkuu
Sio kususa mkuu! Tatizo lako wewe umeitafsiri ktk kunde penzi! Hebu panuka kifikra hayo niliyokwambia hapo juu ndiyo tafsiri stahiki ya neno KIDADA/lubesa/lunyololombi/kitefu nk
 
Sio kususa mkuu! Tatizo lako wewe umeitafsiri ktk kunde penzi! Hebu panuka kifikra hayo niliyokwambia hapo juu ndiyo tafsiri stahiki ya neno KIDADA/lubesa/lunyololombi/kitefu nk
Kwa maelezo ya hizi terms za mwisho sina hoja mkuu
 
"Kidada/shidada" ni kiburi na si kususa! Mfano,"Umwanayu ana kidada/shidada"=Mtoto huyu ana kiburi.
 

Kidada ni kiburi.
 

Ndemngajasida unene
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…