Tabia ya mtoto huyu haifai..

Manyanza

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
16,464
Reaction score
35,629
Wana jamii especially wapenzi wa MMU!

Jana jioni nilimtembelea shemeji maeneo ya Mbezi ya Kawe kwenye flat za BOT...
kituko nilichokiona pale kiliniacha mdomo wazi.

Shemeji analea mtoto ambae alimchukua akiwa ana miezi kumi na moja toka azaliwe baada ya mama wa mtoto kumtelekeza. Ni kitoto cha kike ni kizuri kina afya njema na kicheshi na kichangamfu, umri wake ni miaka 2 na miezi 8.

Jamani nilichojionea jana ni aibu, wakati tukiwa sitting room alikuja jamaa mmoja ambae ni fundi nguo si mnajua baadhi ya mafundi wana mapigo ya kipedeshee suruali mpaka kifuani.

Basi na yule fundi alikuwa kapiga mapigo ya kipapaa alikuwa amekuja kupima nguo za watoto mle ndani akiwa katika process za kupima pima mara alikuwa ana inama yule MTOTO ALICHOFANYA ALIENDA AKAMSHIKA MAKALIO YULE FUNDI (40 YEARS AND ABOVE).

HALAFU MTOTO AKAWA ANASEMA HII ******, nilibaki kinywa wazi na aibu ndani ya nafsi yangu hata yule fundi alijisikia vibaya sana.

Baada ya kuondoka wakina dada walivunja mbavu kwa vicheko wakawa wanasema haaa ndio tabia yake kushika watu hata sisi chumbani huwa anatufanyia hivyo....
ni hayo tu wana MMU...

Hebu fikiria kama angekuwa mtoto wako halafu anafanya kitendo cha aibu kama hicho ungejisikia je?

Halafu na wewe ndiye uliyemuita fundi nguo kuja nyumbani kwako halafu anakutana na madhira kama hayo.
 
duh.... wazazi wake ndio wenye makosa
 
....akamshika makalio yule fundi(40 or above), akawa anasema hii ******
Huyo mtoto hapo kwenye ****** una maanisha alisema 'hii mkwerre?"
 
Reactions: EMT
Depending on malezi, children are likely to follow footsteps of their parents....
 

Hapo nilipobold ndo kuna tatizo, je akiwashikashika wao huko chumbani wanamchukulia hatua gani au na wao wanapenda awashikeshike? Na wewe ulivyoona hivyo ulitoa ushauri gani? hebu waambie wamrekebishe huyo mtoto mapema kabla hajakua bado huu ni mda mzuri wanaweza kumrekebisha na akaacha tabia hiyo.
 
Yaani watu wanacheka badala ya kumfinya na kumzabua mbele ya huyo mgeni,ingekuwa mimi ningemchapa na hyo tabia angekoma,upumbavu kabisa hapo ameanza cku akimshika mwingne kwingne ndo watajua walichofuga,
 
Huyo mtoto hapo kwenye ****** una maanisha alisema 'hii mkwerre?"

Hahaaa haaaaa nadhani alimanisha Makalio(tafsida imetumika) si unajua Mods wanadhibiti matumizi ya maneno makali?
 
Hao walezi hawako serious.. mtoto kufanya hivyo
mbele yao bila negative reaction zaidi ya kucheka sio ustaarabu
na miaka almost mitatu hio hio nafinya huto tumapaja...
 
Haleluya!!! Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo, huyo mtoto alianza kuwashika wenye nyumba chumbani, sasa imefika sebuleni, mhh! Hatua inayofuata mi sielewi endapo huyo samaki hatakunjwa mapema.
 
...she's only a child, an angel! hata hivyo,..."mtoto umleavyo,...!"
 
ndo vitoto vya siku hizi, full kuangalia pilau na wakubwa wao
 
Hayo ni matokeo ya malezi ya one parent, especially akinamama wana tatizo hili sana kiasi nakubaliana na wanaosema "kuzaa si kazi kazi kulea".
 
Reactions: EMT
Mama ni mama. Mtoto halelewi na mama. Unafikiri hao wengine wanacare?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…