Tabia ya muungwana-kutoka kwa mkanyaji

Tabia ya muungwana-kutoka kwa mkanyaji

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
5,497
Reaction score
4,775


TABIA YA MUUNGWANA

Kuno kunena kunena, leo nalinena hili
Nalinena kwa mapana, kwa lugha ya kiswahili
Tabiaze muungwana, si mtu wa ndimi mbili
Kutosheka na akali, tabia ya muungwana.

Nawala hawi mpana, hujiona yu dhalili
Subira imejazana, zimetuwama akili
Kidogo atachovuna, hajipandishi manzili
Kutosheka na akali, tabia ya muungwana.

Ni mbali ametengana, nazo hasira za mali
Hufanya mambo kwa kina, na kukumbuka ayali
Si mambo kujalizana, moyowe huona dhuli
Kutosheka na akali, tabia ya muungwana.

Hasa alo muungwana, si mtamani batili
Uchache kwenye hazina, wala haoni fiili
Hujibanza kwa Rabana, kwa visimamo laili
Kutosheka na akali, tabia ya muungwana.

Na waja atagawana, japo na kiwe kalili
Huwa hapendi kuona, wakinyongeka ahali
Changi ni kuchangizana, hiyo ndioye sabili
Kutosheka na akali, tabia ya muungwana.

Yeye hutafuta Janna, thama kashika adili
Hawi mwenye kujivuna, kwa afanyazo fadhili
Huwa ni mwema msena, kwa matendo na kauli
Kutosheka na akali, tabia ya muungwana.

Hapa tama ya kutona, kalamu yangu mvuli
Wenye macho wataona, hayano yana kulali
Ila walo na hiyana, si lazima kukubali
Kutosheka na akali, tabia ya muungwana.

MKANYAJI
HAMISI A. S KISSAMVU
0715311590/0784311590
kissamvujr@ gmail.com
. kutoka
(Baitu shi'ri)
DAR ES SALAA
 


TABIA YA MUUNGWANA

Kuno kunena kunena, leo nalinena hili
Nalinena kwa mapana, kwa lugha ya kiswahili
Tabiaze muungwana, si mtu wa ndimi mbili
Kutosheka na akali, tabia ya muungwana.

Nawala hawi mpana, hujiona yu dhalili
Subira imejazana, zimetuwama akili
Kidogo atachovuna, hajipandishi manzili
Kutosheka na akali, tabia ya muungwana.

Ni mbali ametengana, nazo hasira za mali
Hufanya mambo kwa kina, na kukumbuka ayali
Si mambo kujalizana, moyowe huona dhuli
Kutosheka na akali, tabia ya muungwana.

Hasa alo muungwana, si mtamani batili
Uchache kwenye hazina, wala haoni fiili
Hujibanza kwa Rabana, kwa visimamo laili
Kutosheka na akali, tabia ya muungwana.

Na waja atagawana, japo na kiwe kalili
Huwa hapendi kuona, wakinyongeka ahali
Changi ni kuchangizana, hiyo ndioye sabili
Kutosheka na akali, tabia ya muungwana.

Yeye hutafuta Janna, thama kashika adili
Hawi mwenye kujivuna, kwa afanyazo fadhili
Huwa ni mwema msena, kwa matendo na kauli
Kutosheka na akali, tabia ya muungwana.

Hapa tama ya kutona, kalamu yangu mvuli
Wenye macho wataona, hayano yana kulali
Ila walo na hiyana, si lazima kukubali
Kutosheka na akali, tabia ya muungwana.

MKANYAJI
HAMISI A. S KISSAMVU
0715311590/0784311590
kissamvujr@ gmail.com
. kutoka
(Baitu shi'ri)
DAR ES SALAA
Mada ya Mja hunena,muungwana ni vitendo
Muungwana amenuna,kachkia zangu nyendo
Muungwana uje nena,utuoneshe upendo
Muungwana sema tena,ufungue hili fundo

Muungwana huna habari,yakuwa mi ndugu yako
Muungwana una Shari,misimamo ndio yako
Muungwana hunijari,yakua mi damu yako
Mada ya ..........._______
 
Back
Top Bottom