Tabia ya ulevi uliokidhiri wa Pombe za Kienyeji kwa Vijana uangaliwe Kagera, naona unachangia kufifisha nguvu kazi ya Taifa

Tabia ya ulevi uliokidhiri wa Pombe za Kienyeji kwa Vijana uangaliwe Kagera, naona unachangia kufifisha nguvu kazi ya Taifa

informer 06

Member
Joined
May 11, 2024
Posts
66
Reaction score
49
Pombe za Kienyeji ni miongoni mwa vyanzo vya mapato ambavyo vimesaidia familia nyingi za 'Nshomile' kupata elimu, leo hii wapo maprofesa, Daktari, Injinia, Walimu na Wafanyabiashara ambao misingi yao ya kuinuka umetokana pombe hizo.

Kwa jamii ya Wanakagera kulingana na mila na tamaduni zilizojengeka kwa muda mrefu vinywaji hivyo (rubisi na konyagi) vimekuwa vikiheshimika huku watumiaji zaidi wakiwa ni watu wazima ambao walikuwa wakizitumia kama kiburudisho zaidi kubadilishana mawazo na mitazamo au katika shughuli za kimila.

Lakini katika hali ya kusikitisha kwa miaka ya hivi karibuni Pombe za Kienyeji ambazo utengenezwa kupitia ndizi za aina mbalimbali zimekuwa tishio na mwiba unaoendelea kuathiri maisha ya watu wengi hususani kundi la vijana kutokana na ulevi unaoendelea kukithiri maeneo mengi ya Mkoa huo.

Nikiwa likizo za sikukuu kwenye Mkoa huo, niliamua kufanya udadisi kwa baadhi ya Kata ambazo zinapatikana kwenye Wilaya za Mkoa huo ikiwemo Wilaya ya Bukoba vijijini, Missenyi na Muleba nimebaini jambo hilo na nimeona sina budi kulibainisha wazi ili hatua za haraka kama zinaweza kuchukuliwa zichukuliwe ili kuleta ustawi.

Kupita watu na vyanzo nilivyozungumza navyo inaonesha kwenye Kata takribani 10 ambazo nimepata kufanya udadisi huu, kuna wastani wa vifo viwili hadi vinne kila mwaka ambavyo vinatokana na matumizi ya pombe yaliyokithiri (ulevi).

Niliguswa kuanza kufanya udadisi huo mara baada ya kusikia vifo vingi vinavyoripotiwa vikihusishwa na ulevi, huku kundi la vijana ambao ni nguvu kazi ya Taifa wakiwa waathirika wakubwa.

Hali hiyo imeanza kubadili mitindo ya maisha ya vijana wengi pamoja na jamii kwa ujumla huku ikichangiwa na suala linaloibuka kwa kasi la uvutaji wa ugoro, ambapo katika kufuatilia inaelezwa kuwa umekuwa ukisambazwa na mtandao unahusisha baadhi ya watu kutoka Nchi jirani ya Uganda ambapo unadaiwa kutokea kupitia maeneo ya mipaka kwenye Wilaya ya Missenyi.

Katika mazingira hayo kundi kubwa la vijana lipo hatarini kuathirika huku nguvu kazi ya Taifa ikizidi kupotea na suala la mmomonyoko wa maadili likiendelea kupolomoka kwa kasi kubwa.

Hali hii inaongeza kwa kasi uwezekano wa watu kushindwa kuwajibika ipasavyo kutokana na afya zao kwa wingi kuwa goigoi. Hata hivyo inapelekea ushiriki wa vijana kwenye masuala ya maendeleo ya kijamii kuwa duni jambo ambalo sio rafiki kwa ustawi wa jamii ya kesho.

Katika kujua ni hatua zipi zinachukuliwa na mamlaka pamoja na jamii kwa ujumla, vyanzo mbalimbali vinanitonya kwamba kumekuwepo na zuio kwa maeneo ya starehe hususani bar na vilabu vya pombe kutofunguliwa muda wa kazi.

Halmashauri zimekuwa na utaratibu huo kwamba maeneo hayo yafunguliwe baada ya muda wa kazi (saa tisa na kuendelea), lakini katika maeneo mengi utaratibu huo inabainika hauzingatiwi ipasavyo.

Licha ya utaratibu huo zinahitajika mbinu za ziada kwa Halmashauri na mamlaka nyingine kuweka mikakati ya kuelekeza elimu kwa vijana juu ya namna ambavyo wanaweza kuepuka mazingira ya kuingia kwenye ulevi uliokithiri huku viongozi wa dini na viongozi wa kijamii wakiwa sehemu ya utekelezaji wa mikakati hiyo.

Sanjari na hayo nitoe rai kwa mamlaka zifuatilie madai kuhusu mawakala wanaosambaza ugoro ambao kwa sasa umekuwa mwiba kwa afya za vijana wengi.
 
Back
Top Bottom