Tabia ya vyuo vya elimu ya juu kufundisha certficates na diplomas inapoteza dira ya elimu!

mahwelu

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2013
Posts
322
Reaction score
253
Wakuu wana JF hasa wenye thinking capacity na maono ya mbali naomba mliangalie hili kwa upeo wake. Mimi sio mtaalamu sana wa masuala ya elimu but nimekuwa nikidadisi kiasi tu. Leo niomba tuchambue tabia ya vyuo vya elimu ya juu kuchukua wanachuo wa katika ngazi ya vyeti na diploma. nimefuatilia ni kwamba karibuni vyuo vingi vya eleimu ya juu vimeingia kuanzisha kozi na kuchukua wanafunzi wengi katika vyuo vyao kiasi cha kuacha vyuo vya kati vikikosa wanachuo.
Najua hadi hapa sijamake sense kwa wengi but nataka kuongeza kwamba hapo kabla elimu yetu ilikuwa na dira na malengo halisi. tulikuwa na shule za secondari na msingi kama source ya elimu then tukawa na vyuo vya hadhi mbali mbali - vile vyenye kutoa professional trainings kama DIT, Mzumbe, IFM, DSA, etc.. then tulikuwa na vyuo vikuu halisi kama UDSM, SUA NK. mafunzo , dhamira na style za kutoa elimu katika vyuo hivi pia yalitofautiana. vyuo vikuu vililenga kutoa critical thinkers katika fani mbali mbali na njia iliyotumika kufundisha ni mihadhara (lecture). hivi vyuo vingine vililenga kutoa watendaji katika fani mbali mbali na ndio maana mtu alikuwa akimaliza Dar tech anatakiwa aweze kufanya kile alichosomea but kwa aliyetoka UDSM anatakiwa kuwa na analytical skills katika fani.

Kinachtokea sasa ni kwamba vyuo vinachukua vijana katika level za vyeti na diploma na kuwapa elimu kama vile wanawafundisha wanachuo wenye level ya degree. malengo ya vyuo hasa ni mawili; kuongeza kipato na pia kuwaandaa kwa ajili ya kujiunga na elimu ya juu. najua kwa wenye maono mnajua niendako nako ni kwamba tunapoteza kada ya watendaji sasa hivi... diploma za vyuo hivi hazina tija kama mwanao hakufuzu kuingia degree...

sababu ambayo vyuo wamefikia hapo ni kipato katika level mbili: kwanza ni application fees kwani vyuo vimepoteza mtaji kwa TCU tangu waanzishe online regestration. so kupitia diploma bado vyuo vinapata 30 30k za applicants.. totak ni average ya 200Mil wa vyuo kama udsm. Pia kuwepo kwa certificates na diploma kunasaidia kupoteza malengo ya serikali kwani hawa watu hawapitii loans boards ambapo vyuo vinacheleweshea mapato . hawa wanalipa cash kwa mkono.. wow kwa vyuo.

Naomba wakuu tuangalie madhara kwa taifa na tutafute jinsi ya kukemea. kwangu naona bor avyuo vile vile kama bagamoyo -SLADs, dsa - TIA products zao zinafaa. kwani kuandika vocha anahitajika degree holder wanini?

ni hayo tu wakuu!!! hasa kwa wenye maono na great thinkers sio wakurupukaji.

with thanks!!
Nangu mahwelu
 
Mtu anamaliza diploma ya IT kameza definitions tu, hajui hata kufanya backups katika database..elimu kwa certificates na diploma imekuwa ya dalasani sana na sio practical, watu wanasoma ili wapate pasi kubwa waingie digri na sio kupata ujuzi
 

some how true ...!
 
Mi sidhan kama itaathili kwa sababu si kila level ina eneo lake? licha ya kuwa ndan ya vyuo vikuu, kwanza hii inasaidia zaid kwa wanaochukua certificate/diploma kupata mwelekeo wa maendeleo yao ya kimasomo kwa sababu watayajua mazingira ya elim ya juu mapema. sasa labda utueleze itaathili vp hebu fafanua mkuu.
 
Mtu anamaliza diploma ya IT kameza definitions tu, hajui hata kufanya backups katika database..elimu kwa certificates na diploma imekuwa ya dalasani sana na sio practical, watu wanasoma ili wapate pasi kubwa waingie digri na sio kupata ujuzi

mkuu mimi kwa uelewa wangu nadhani kama ulivyosema, kinyume chake ni sahihi kwa sababu muundo wa utaratibu wa kujifunza kwa ngazi ya diploma ni tofauti kidogo na degree hivyo diploma wanakuwa competent sana kiutendaji ukilingananisha na degree. Namaanisha wana muda wa kutosha kujifunza vitu tofauti na vyuo vikuu vinavyochukua course units kwa masaa machache
 
ahaa haya mi napita tu umenena lakini!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…