Davidmmarista
JF-Expert Member
- Apr 11, 2024
- 1,367
- 2,451
Wadau wa Jamiiforums, Salamu Zenu!
Kama kuna kitu kipo wazi kama jua la mchana ni kwamba mafogo (matajiri) wanafikiria tofauti na sie wa kawaida. Kuna watu wanasema eti "tajiri akisema ni mchana hata kama ni usiku, huna haja ya kubisha, tafuta sababu ya kwa nini anasema hivyo!"
Lakini je, umewahi kujiuliza ni kwa nini matajiri wanaendelea kuwa matajiri kila siku? Je, kuna siri wanazojua na sisi maskini hatujui? Hapa leo nakuletea tabia zao zile zinazowafanya waendelee kupiga pesa, wakati wengine tunabaki na ndoto tu za "kimoja kimoja kinaelekea."
Ukisoma huu uzi mpaka mwisho, hautaangalia pesa kwa mtazamo ule ule tena. Tena kama upo serious, unaweza kubadilisha kabisa maisha yako! Basi, twende moja kwa moja kwenye tabia zao mafogo ambazo zinawafanya waendelee kuwa mafogo.
1. Mafogo Wana Ndoto Kubwa Kuliko Maisha Yao ya Sasa
Mafogo hawapangi mipango midogo. Wakati wewe unawaza namna ya kumiliki bodaboda, wao wanafikiria kufungua kampuni ya usafiri wa anga.
Mfano halisi ni Elon Musk, wakati watu wanafurahia magari ya mafuta, yeye akawa na wazo la magari yanayotumia umeme (Tesla). Wakati watu wanaona kuwa safari za anga ni kwa NASA tu, yeye anapanga kuwapeleka watu Mars!
Ukiwa mtu wa kawaida unawaza hivi:
"Mwaka huu nitatafuta boda boda angalau niwe na kitu."
"Nikipata kamtaji ka milioni mbili nitafungua genge au nirushe hapo dukani chap."
Mafogo wanawaza hivi:
"Nataka kumiliki kampuni ya usafirishaji wa ndege ndani ya miaka mitano."
"Nataka kuwa na mnyororo wa maduka 50 ndani ya miaka mitatu."
"Go big or go home." – Mafogo
2. Mafogo Wanathamini Muda Kuliko Pesa
Kuna msemo maarufu unasema:
"Maskini huuza muda wake kwa pesa, tajiri hutumia pesa kununua muda."
Kwa mfano, wewe unaweza kusema:
"Nataka kutoka Kariakoo hadi Masaki, acha nitumie daladala nipunguze gharama." (Dakika 120 barabarani)
"Acha nipike mwenyewe ili nisiagize chakula." (Dakika 60 jikoni)
Mafogo wao hufikiria hivi:
"Nikichukua Uber badala ya daladala, nitafika mapema na kuokoa muda wa kufanya kazi nyingine yenye pesa."
"Badala ya kupika, bora niagize chakula ili niendelee kupanga mikakati ya biashara."
Mafogo wanajua kuwa muda ni wa thamani kuliko pesa, na ndio maana wanawekeza kwenye vitu vinavyowaongezea muda wa kufanya mambo makubwa zaidi.
3. Mafogo Wanapenda Kujifunza Kila Siku
Ukiingia kwenye nyumba ya fogo wa ukweli, huwezi kukosa maktaba. Wana vitabu kibao vya biashara, uwekezaji, na hata falsafa za maisha, ukifungua simu zao au computer zao ni maudhui ya kujifunza.
Mfano mzuri ni Bill Gates, tajiri ambaye husoma vitabu 50 kwa mwaka. Wewe unasoma ngapi?
Wakati wewe unakesha ukimaliza "Season 10 ya Money Heist" mafogo wanakesha wakisoma vitabu kama:
- The Richest Man in Babylon
- Think and Grow Rich
- The Intelligent Investor
"Ukiona maskini wa akili, jua akili yake imechoka kusoma." – Mafogo
4. Mafogo Hawapendi Kujionesha Ovyo (Wanapenda Low-Key Life)
Wakati mtu wa kawaida akipata pesa kidogo anaenda Instagram kupost:
"Finally, hard work pays off! Blessed."
Mafogo wao wanaingiza mamilioni lakini wapo kimya.
Mfano: Angalia matajiri wakubwa kama Warren Buffett mzee ana pesa ya kununua nchi lakini anaishi kwenye nyumba aliyoinunua miaka ya 1950 kwa $31,500 tu!
Wewe bado hujatoboa, lakini kila hela inayoingia unapiga picha na caption ya "God Did!"
Mafogo wanajua kuwa pesa hupenda utulivu. Ukianza kupiga kelele sana, utajikuta kwenye rada za watu wasiokutakia mema.
5. Mafogo Wanapenda Kutengeneza Pesa Hata Wakiwa Wamelala (Passive Income)
Mtu wa kawaida anafanya kazi ili apate pesa. Mafogo wanajenga mfumo wa pesa kufanya kazi kwa ajili yao.
Mfano:
Mtu wa kawaida: Anaenda kazini saa 2 asubuhi, anarudi saa 11 jioni. Hakitokea kitu kama ugonjwa au likizo, hana kipato.
Fogo: Ana maduka, ana biashara ya Airbnb, ana hisa, na ana uwekezaji. Hata akiwa amelala, pesa inaingia.
"If your money is not working for you, then you will always have to work for money." – Mafogo
6. Mafogo Wanahifadhi na Kuwekeza Pesa, Sio Kuzitumia Ovyo
Kuna msemo wa mafogo unasema:
"Maskini anatumia pesa kwanza, kilichobaki anaweka akiba. Tajiri anaweka akiba kwanza, kilichobaki anatumia."
Mfano mzuri ni Mark Zuckerberg ana mabilioni lakini bado anavaa t-shirt ya rangi moja kila siku. Lakini mtu wa kawaida akipata pesa kidogo lazima ajilipue na Gucci fake!
7. Mafogo Hawapendi Madeni Yasiyo na Faida
Wakati sisi tunakopa hela kwenda kufanya sherehe ya birthday na kununua iPhone mpya, mafogo wanakopa pesa kuwekeza kwenye biashara.
"Debt is a powerful tool, but only if used wisely." – Mafogo
8. Mafogo Wanaogopa Kukaa na Watu Wasiokuwa na Maono
Wewe unashinda na watu wanaoongelea siasa na umbea wa mtaa. Mafogo wanashinda na watu wanaoongelea biashara, uwekezaji, na fursa mpya.
"If you want to be rich, hang out with people who talk about making money." – Mafogo
9. Mafogo Wanapenda Kujaribu Mambo Mapya Bila Kuogopa Kupoteza
Wakati mtu wa kawaida anaogopa kupoteza pesa, mafogo wanajua kuwa kila biashara ni risk. Wanajaribu, wanakosea, wanajifunza, halafu wanarudi kwa nguvu mpya.
Mfano ni Jeff Bezos alipoanzisha Amazon, watu walimcheka wakisema biashara ya kuuza vitabu mtandaoni haitafanikiwa. Leo hii, Amazon ni moja ya makampuni yenye thamani kubwa zaidi duniani!
"Success is a series of failures, but the difference is learning from each one." – Mafogo
10. Mafogo Wanajua Kujiongeza Bila Kuingia Katika Rushwa au Njia Chafu
Wengi wanadhani kila tajiri ni mwizi. Ukweli ni kwamba mafogo halisi wanajua jinsi ya kujiongeza kisheria. Wanatafuta mbinu za kutumia sheria zilizopo kuwafanya waendelee kupiga pesa.
Mfano: Badala ya kukwepa kodi, mafogo wanajua jinsi ya kutumia "tax loopholes" kihalali. Badala ya kuomba rushwa, wanajua jinsi ya kutengeneza thamani inayowafanya wapewe mikataba mikubwa bila hila.
"Smart people find ways to win legally. The lazy ones blame the system." – Mafogo
Hitimisho: Kama Unataka Kuwa Fogo, Badilisha Mtazamo!
Jiulize Leo.
- Je, nina mipango mikubwa au nipo tu bora liende?
- Je, ninapoteza muda wangu kwa mambo yasiyo na faida?
- Je, ninawekeza katika kujifunza kila siku?
- Je, napanga pesa yangu vizuri au naishi kwa mshahara hadi mshahara?
- Je, nazungukwa na watu wa aina gani?
Kama majibu yako yanaonyesha unaishi kama mtu wa kawaida, basi tambua: “Kama utaendelea kufanya mambo yale yale, utapata matokeo yale yale.
Mafunzo ya kuchukua:
• Waza mambo makubwa.
• Tumia muda vizuri.
• Jifunze kila siku.
• Acha kujionesha ovyo.
• Tengeneza passive income.
• Hifadhi na wekeza pesa zako.
• Acha madeni yasiyo na faida.
• Chagua marafiki wenye maono makubwa.
NB: Naomba radhi sana leo katika upangiliaji wangu wa kazi, sijapangilia vizuri, lakini ni matumaini yangu kuwa kila mmoja amepata kitu cha kujifunza.