Tabia za wakulima zinazosababisha kilimo kisiendelee

Tabia za wakulima zinazosababisha kilimo kisiendelee

Kamgomoli

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2018
Posts
1,896
Reaction score
4,058
Bila kupoteza muda zifuatazo ni tabia za wakulima zinazofanya kilimo kisiendelee:-

1.Kulima bila kufanya maandalizi. Wakulima wengi hawafanyi maandalizi mapenda yaani wanasubiri mvua inyeshe ndo waanze kusafisha shamba,kutafta mbegu na mbolea.Matokeo yake wanaelemewa na kazi au kushindwa kuhudumia shamba kikamilifu.

2. Wanasuburi taarifa za kitaalamu ziwafate nyumbani. Wakulima wengi hawapendi kujiongeza kufuata taarifa za kitaalamu kwa kupiga simu au kufuata taarifa sahihi kwenye vituo vya utafiti hata km viko jirani yao. Wamebaki kulaumu eti wataalamu hawawatembelei utadhani wakivuna mazao watagawana.

3.Kulima kwa mazoea.
Hata km wakishauriwa vipi, wakulima wa kitanzania ni wagumu mno kubadilika. Mfano wengi wameng'ang'ania kulima mahindi wakati mbolea bei iko juu mno wakati uzalishaji wa Alizeti na maharage ni "cheap".

4.Kulima bila malengo.
Wakulima wengi hawalimi kwa malengo.Unakuta msimu wa mvua unaanza mkulima hajui atalima nini na kwa kiasi gani. Yaani bora liende.

5.Kulima bila kuzingatia soko.
Alime nini kwa wakati gani na atamuuzia nani? Mtu anajilimia tu bila kujua atauza wapi.

6. Kulima kwa kuigana. Ikitokea mtu kalima nyanya akauza vizuri basi wote wanakimbilia kwenye kilimo cha nyanya. Matokeo yake ni nyanya kulimwa kwa wingi na kukosa soko.

Ni hayo tu.
 
Lawama ulizotupa ni haki yetu/zinatustahili.
Tumekuelewa na tunashukuru.
Je Hakuna mema tufanyalo au jema tunalostahili kufanyiwa na jamii isiyo ya wakulima au kufanyiwa na serikali?
 
Back
Top Bottom