Najisi asili yake ni neno la Kiarabu na nitakapotoa tafsiri au maana zake si vema kuingiza udini. Maana ya kwanza na itumikayo sana ni uchafu ila huo uchafu nao una aina nyingi labda Kiingereza kitasaidia kutoa mwangaza: dirty, filth, impure, profane, contamination. Pia ipo najisi kitendo - (verb) k.m. kumnajisi mwanamke (defile or rape a woman).
Najisi kwa Uislamu (ritual uncleanliness) zipo aina nyingi vile vile lakini kwa muhtasari tu zinagawika kama najisi ndogo na najisi kubwa. Najisi kubwa ni ile ambayo Muumini akiwa naye au akiipata ni budi aoge udhu wake ukamilike, kama vile akifanya kitendo cha ngono, kutokwa na manii au kuchezea sehemu za siri za opposite sex, n.k. Lakini najisi ndogo (kwenda haja kubwa au ndogo, n.k.) udhu unaweza kupatikana kwa kutawadha tu, yaani kujiosha viganja vya mikono, mikono yenyewe, pua, uso na miguu. Baada ya kutakasika (kuzitoa hizo najisi) ndio Muumini anaruhusiwa kuswali, kushika Msahafu (Qur'an) na kufanya ibada zingine.
Swali lako naona limeambatana na picha ya Ferry huku mtu anakojoa baharini na mwingine anapaa samaki. Hiyo ni najisi anatia baharini lakini mimi sitatoa ufafanuzi iwapo hao samaki ni "halali", wasafi kuliwa au ni najisi pia! Nawaachia wenzangu wajuzi zaidi wachangie hii mada.