Tabibu akamatwa kwa kumuomba mgonjwa rushwa na kufanya upasuaji asio na ujuzi nao

Tabibu akamatwa kwa kumuomba mgonjwa rushwa na kufanya upasuaji asio na ujuzi nao

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
1579582474226.png

Katika hali ya kushangaza Tabibu Msaidizi Eliud Humbo anashikiliwa na Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) baada ya kufanya upasuaji asio na ujuzi nao

Humbo ambaye andaiwa kumfanyia Upasuaji wa ngili mgonjwa mmoja ambaye alipewa rufaa ya kwenda hospitali ya mkoa

Mkuu wa Mamlaka hiyo mkoani Rukwa Hamza Mwenda amesema kuwa mgonjwa huyo alikutana na mtuhumiwa wakati anajupanga kwenda hospitali

“Awali mgonjwa huyo alibainika kusumbuliwa na ugonjwa wa ngiri na madaktari walimpatia rufaa kwenda kutibwa katika Hospitali ya Mkoa wa Rukwa iliyopo katika Mji wa Sumbawanga Wakati akijiandaa kutoka katika Kituo cha Afya Matai ili akatibiwe mjini Sumbawanga alikutana na Humbo ambaye alimhakikishia kuwa ana uwezo wa kumfanyia upasuaji na atapona huku akitakiwa kutoa kiasi cha pesa shilingi laki moja (100,000) ili kufanyiwa upasuaji huo” amesema.

Baada ya mtuhumiwa kupokea fedha hizo kutoka kwa mgonjwa huyo, alikwenda kwa Msimamizi wa Kitengo cha Tohara kwa wanaume akidai ana mgonjwa aliyekuwa akihitaji kutahiriwa.

“Mtuhumiwa huyo alikabidhiwa vifaa vilivyohitajika kwa kumfanyia tohara mgonjwa wake, lakini alimfanyia upasuaji wa ngiri kwa kumpasua tumbo lake,’’ alisema.

Mgonjwa anapelekwa hospitali ya mkoa kwa matibabu zaidi mara baada ya utumbo wake kutolewa nje kwa muda kadhaa kutokana na tabibu huyo kushindwa kumalizia upasuaji
 
Njaa mbaya kwa madaktari, hapo alikuwa anajaribu kupata chochote kitu.
 
Back
Top Bottom