Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Jimbo la Magharibi Tabora, Isaac Laizer, ameonya juu ya ongezeko la matukio ya utekaji na mauaji, akiwataka wakristo kote nchini kufunga na kuomba kwa dhati ili kutokomeza matukio hayo.
Akizungumza jana, Desemba 8, 2024, katika maombi ya kitaifa ya vijana yanayoendelea mkoani Tabora, Askofu Laizer amesema Taifa linakabiliwa na changamoto kubwa na maombi ya pamoja ni njia muhimu ya kufanikisha mabadiliko.
"Endapo maombi hayatafanyika kwa dhati, nchi yetu itaendelea kupitia kipindi kigumu. Tunapaswa kuungana kwa maombi ili kutokomeza utekaji na mauaji yanayoshika kasi," amesema Laizer.
Pia, amewataka wakazi wa Tabora kuachana na fikra za kutegemea miujiza badala yake wafanye kazi za kuwaingizia kipato. "Mkoa wetu unaongoza kwa watu kutosimama kidete kujitafutia maendeleo, hali inayorudisha nyuma juhudi za maendeleo ya kiuchumi."
Pia, Soma:
• Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) yakemea vitendo vya utekaji, ukatili na mauaji yanayoendelea nchini
• Askofu Shoo akemea vitendo vya kikatili vinavyohusisha mauaji, utekaji na matumizi mabaya ya nguvu na mamlaka
• Askofu Dkt. Malasusa: Mambo ya Utekaji yafike mwisho nchi inalaanika Damu zinavyomwagika, Dkt. Biteko Wanasiasa kaeni chini msikilizane!