Tabora Hotel alipohojiwa Bilal Rehani Waikela 1969

Tabora Hotel alipohojiwa Bilal Rehani Waikela 1969

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
TABORA HOTEL MAHALI ALIPOHOJIWA SHEIKH BILAL REHANI WAIKELA BAADA YA "MGOGORO" WA EAMWS 1969
''Kilichobakia baada ya kuvunjika kwa EAMWS ilikuwa ni kujaribu kuiweka BAKWATA katika mikoa kama jumuiya inayowakilisha Waislam wote wa Tanzania Bara.

Mwaka mzima wa 1969 Adam Nasibu na kamati ya watu wanne walitembea katika mikoa wakiahidi msaada wa fedha kwa katibu yeyote wa zamani wa EAMWS ambae atashirikiana na BAKWATA makao makuu kuisaidia kufungua ofisi katika mkoa wake.

Waislam waliipuuza BAKWATA.

Tabora ambayo haikujitoa katika EAMWS, serikali iliwaruhusu Adam Nasibu na kikundi chake kufanya mkutano wa hadhara.

Kabla Adam Nasibu hajahutubia Waislam, Maulid Kivuruga mmoja wa wakongwe wa African Association na muasisi wa TANU Tabora, alipanda jukwaani kwa niaba ya Waislam wa Tabora na kuweka sharti kuwa Waislam watakuwa tayari kumsikiliza Adam Nasibu endapo Waikela mjumbe wa Tume ya Waislam iliyokuwa ikitafuta sulhu na yeye ataruhusiwa na serikali kuwahutubia Waislam ili aeleze upande wa pili wa kisa kile.

Kivuruga alisema kuwa Waislam wanaomba sharti hili likubaliwe kwa sababu katika Uislam panapotokea mgogoro basi mpatanishi ni lazima asikilize pande zote mbili.
Sharti hili lilikataliwa na BAKWATA na serikali.

Palepale mbele ya waheshimiwa wa serikali na viongozi wa BAKWATA, Waislam wakaanza kuzomea huku wakitawanyika wakipiga takbir na wengine wakiitikia Allahu Akbar.

Siku chache baada ya tukio hili Waikela aliitwa na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Jinai kusailiwa kwa nini anaipinga BAKWATA.

Wakiwa ndani ya chumba cha Tabora Hotel, Mkrugenzi wa C.I.D, alimpiga maswali Waikela na kutaka kujua kwa nini yeye hayuko tayari kushirikiana na serikali kuipa nguvu na kuieneza BAKWATA.

Sawaya akatoa hongo ya shilingi elfu arobaini kwa Waikela ili asaidie kuimarisha BAKWATA.
Waikela kama istizai alimuuliza Sawaya kama fedha zile zilikuwa zimetoka ''Bait Mal.''

Waikela alikataa kupokea hongo ile.
Akamtishwa lakini Waikela hakutishika.

Waikela aliwekwa ndani ya chumba kile akiulizwa maswali kwa kiasi cha saa nne na kisha akaamrishwa kuweka sahihi yake katika makaratasi fulani.

Hili alilifanya.
Waikela hakufuatwa tena na serikali.

Ingawa kulikuwepo na juhudi za chinichini za kuipinga BAKWATA, juhudi hizi hazikushinda kwa kuwa BAKWATA iliweza kufungua matawi yake nchi nzima pamoja na Tabora.

Wapo baadhi ya viongozi ambao hawakuweza kuhimili vishawishi vya kupokea ile hongo ya serikali na kwa ajili hii walishirikiana na serikali hivyo kuwezesha ofisi za BAKWATA kufunguliwa, hata kama zipo pale kwa jina tu.''

(Kutoka kitabu cha Abdul Sykes 1998)

Huyu ndiye Bilal Rehani Wakela.

Allah msamehe makosa yake na mtie peponi.
Amin.
1657564350199.png

1657564376159.png
1657564407524.png
 
Back
Top Bottom