Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 6,067
- 10,938
Watoto wawili wa familia moja katika kijiji cha Usuhilo Manispaa ya Tabora, wamefariki dunia kwa kukosa hewa ya kutosha baada ya wazazi wao kuwasha jiko la mkaa na kuliweka ndani ili waote moto na kujikinga na baridi. Watoto waliofariki ni Amani Athumani, (1) na Zainabu Athumani (1). Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora ACP Richard Abwao amesema tukio hilo limetokea February 5, 2022 majira ya saa 6 usiku
Baba wa Watoto hao Athumani Shabani (45), Mkewe Magreth Joseph (34) pamoja na Neema Athumani (17) wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora Kitete kutokana na kuathirika kwa kukosa hewa pia kulikosababishwa na jiko hilo la mkaa na hali zao sio nzuri.
Sababu zinazoweza kusababisha kifo kutokana na jiko la mkaa. soma Kwanini jiko la mkaa ukiwa ndani linaweza kupelekea vifo
Visa mbalimbali vya vifo vitokanavyo na jiko la mkaa

- Geita: Jiko la mkaa laua Mama, watoto wawili
- Jiko la mkaa laua tena Njombe ni baada ya mwingine kulala na jiko kwenye kibanda cha biashara
- Njombe: Wapenzi wafariki wakiwa wamelala chumbani na jiko la mkaa