Tabora: Kata ya Imalamihayo - Uyui maji yapo, bado gati moja katika kitongoji, kazi itakamilika Januari

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Baada ya Mdau wa JamiiForums kudai kwamba Wananchi wa Kata ya Uyui iliyopo mkoa wa Tabora kuwa hawajawahi kupata maji ya Bomba tangu Nchi ipate uhuru,(DOKEZO - Inadaiwa Wananchi wa Kata ya Uyui kuwa hawajawahi kupata maji ya Bomba tangu Nchi ipate uhuru), Waziri wa Maji Juma Aweso amesema Maji yapo. "Manispaa ina Kata 29 ikijumuisha Kata ya Uyui. Kata zote 29 zimeshafikiwa na huduma ya maji.

Soma hapa chini Majibu ya Waziri Aweso

Manispaa ya Tabora ni moja ya maeneo ambayo imeshafikiwa na maji ya ziwa victoria.

Manispaa ina Kata 29 ikijumuisha Kata ya Uyui. Kata zote 29 zimeshafikiwa na huduma ya maji.
Kata ya Uyui ambamo kijiji cha Imalamihayo kimo ina jumla ya magati 14 ambapo, magati 13 yanatoa maji na Gati moja (1) lipo kwenye hatua ya kukamilishwa kufungiwa Bomba.

Kijiji/Mtaa wa Imalamihayo pekee kina magati matatu (3).
Magati mawili (2) yana maji na Gati moja (1) liko kwenye mradi unaoendelea wa kulaza Bomba kufikia eneo hilo.

Wizara ya maji kupitia Mamlaka ya majisafi na Usafi wa Mazingira Tabora (TUWASA) inatarajia kukamilisha mradi huo mapema mwezi Januari, 2025.

WAZIRI WA MAJI
JUMAA AWESO
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…