Mpekuzi Tanzania
JF-Expert Member
- Mar 11, 2018
- 650
- 1,016
MJUMBE WA KAMATI KUU YA CCM ATUA IGUNGA, AONGEA NA WANACHAMA NA KUKAGUA UJENZI WA WODI YA MAMA NA MTOTO
"Katibu wa CHADEMA Jimbo la Igunga, aunga mkono juhudu za Mama Samia na kuhamia CCM"
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Mlezi wa Mkoa wa Tabora Ndg. Afadhal Taibu Afadhal (MNEC), Leo tarehe 14 Oktoba 2021 amefanya ziara Wilaya ya Igunga, Mkoa wa Tabora.
Ziara ya Ndg. Afadhal Taibu Afadhal (MNEC) akiwa ameambata na Viongozi wa CCM Mkoa, Viongozi wa CCM Wilaya, Mbunge wa Jimbo la Igunga Mhe. Nicholaus George Ngassa, Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Burian, Mkuu wa Wilaya ya Igunga Mhe. Sauda Mtondoo na Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Ndg. Othman Masoud (MNEC) imeanzia Hospitali ya Wilaya kwa ajili ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Wodi kubwa ya kisasa ya uzazi (Mama na Mtoto) inayojengwa na Serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa gharama ya Fedha kiasi cha Shilingi Milioni Mia Moja na Sabini na Saba (Tshs 177,000,000) kwa programu ya kulipa kwa matokeo (Result Based Financing).
Baada ya ukaguzi wa Wodi ya Mama na Mtoto, Ndg. Afadhal (MNEC) amekutana na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Wilaya wa Jimbo la Igunga na Wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwenye kikao cha ndani kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya.
Katika kile kinachoonekana na kuvutiwa na utendaji wa Serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM) inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan, Katibu wa CHADEMA Jimbo la Igunga Bw. Jumanne Yusuph (Baba Jiwe) ameamua kuunga mkono juhudu za maendeleo na kuhamia CCM. Bw. Jumanne Yusuph amepokelewa na Ndg. Afadhal (MNEC) nakutakiwa kufuata taratibu zote za kujiunga rasmi na Chama cha Mapinduzi (CCM).
"Kazi na Maendeleo"