Tabora: Marufuku kuuza majeneza hadharani

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Mkuu wa Mkoa wa Tabora ametoa miezi mitatu kwa halmashauri zote mkoani hapo, kutenga maeneo yatakayokuwa na miundombinu ya kujificha ya kutengeneza na kuuzia masanduku ya kuzikia maiti (majeneza) kwani kwa sasa wauzaji wa masanduku hayo wanayauzia hadharani kando na hospitali hali inayoongeza hofu kwa wagonjwa na baadhi yao hupoteza maisha na wengine wanapata magonjwa ya akili.

Hata hivyo, wauzaji wa majeneza hayo wamekiri kuwa uuzwaji wa masanduku hayo katika maeneo ya wazi karibu na hospitali inaogofya wagonjwa na ndugu zao na kuunga mkono mpango huo wa Serikali.

Soma Pia: Majeneza getini mwa Hospitali ya Amana hayaleti taswira nzuri kwa Wagonjwa.

Chanzo: Radio One
 
Kwakuwa watu wa tabora hawafi .Na mifano ipo yupo mwamba wa masasi 30 na akakwepa kifo.Hongera watu wa tabora a.ka nyuki.
 
Kwa jamii iliyostaarabika hii si biashara ya kufanyia hadharani au jirani na hospital. Wakati watu wanaingia hospital kupambania uhai wao. Wauzaji wao wanatamani/ikibidi wanaloga wagonjwa wafe wapate hela.
Hii siyo sawa. Yawekwe maeneo maalumu kwa biashara hiyo,tena isiwe open space.
 
Ni kweli watu wa Tabora wanaweza kukuhujumu hata kwa kukuroga au MAKAFARA ili wauze majeneza vizuri

Hatari SANAA
 
Wamechelewa sana kupiga stop ,muhimbili walifanya hvyo miaka karibia 10 iliyopita.
 
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Chacha amemuagiza katibu tawala wa mkoa huo kutenga maeneo maalumu kwa ajili ya wafanya biashara wa majeneza ili waondoe shughuli zao nje ya Hospitali ya Kitete.

Amesema kuendelea kufanya biashara hiyo maeneo hayo tena hadharani, kunatajwa kuongeza hofu kwa wagonjwa wanaopelekwa kupata matibabu pindi wayaonapo yamepangwa nje.

Mkuu huyo wa mkoa ameyasema hayo leo Jumanne Novemba 5, 2024 baada ya kutembelea hospitali hiyo ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora na kushuhudia wafanya biashara wa majeneza wakifanya shughuli zao mbele ya lango kuu la hospitali hiyo.

Chacha amesema kuna baadhi ya wagonjwa wanaweza kukata tamaa na kuingiwa na hofu baada tu ya kuona jeneza mbele yake.
 
Back
Top Bottom