Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Mkoa wa Tabora unapatikana katikati ya Tanzania, unapakana na mikoa ya Shinyanga, Singida, Kigoma, Katavi, na Mbeya. Mkoa wa huu una ukubwa wa takriban kilomita za mraba 76,151, na ni miongoni mwa mikoa mikubwa zaidi nchini Tanzania.
SOMA PIA
Idadi ya Watu
Kulingana na Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022, Mkoa wa Tabora una jumla ya watu 3,391,679. Idadi hii inajumuisha wanaume 1,661,171 na wanawake 1,730,508, na mkoa huu una jumla ya wilaya 8.
Mkoa wa Tabora una jumla ya Majimbo 8 ya kiuchaguzi yaliyogawanyika katika wilaya 8, Majimbo hayo ni:
- Nzega Mjini
- Bukene
- Nzega Vijijini
- Igunga
- Manonga
- Igalula
- Tabora Kaskazini
- Urambo
- Sikonge
- Tabora Mjini
- Kaliua
- Ulyankulu
Uchaguzi Mkuu 2020, CCM ilishinda nafasi zote za Ubunge ndani ya Mkoa wa Tabora, Katika maeneo mengi, wagombea wa CCM walipita bila kupingwa kutokana na vyama vya upinzani kutokidhi vigezo kwa sababu zilizotolewa kuwa walikosea kujaza fomu au kuchelewa kurejesha fomu na wengine kujiondoa kwa sababu ya kile walichoeleza kuwa ni mazingira yasiyo ya haki kwenye mchakato wa uchaguzi.
Kwa upande wa Nafasi ya Urais CCM ilishinda nafasi hiyo kupitia Mgombe wake Hayati John Pombe Magufuli ambaye alishika nafasi hiyo mpaka mwaka 2021 ambapo Alifariki Dunia na kisha nafasi ya Urais kushikwa na aliyekuwa Makamu, Rais Samia Suluhu Hassan.
Soma Pia:
Januari
- CHADEMA Sikonge: Watakaoihujumu "No reforms No election" hawatavumiliwa
- Pre GE2025 - Tabora: Wananchi Wampongeza Dkt. Samia, Dkt. Mwinyi na Dkt. Nchimbi kwa Kugombea Urais 2025
- Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii yaridhishwa na ujenzi wa mradi wa maktaba ya Chuo cha Ardhi Tabora (ARITA) uliofikia asilimia 99
- Pre GE2025 - Baada ya Samia Legal Aid sasa wameanzisha "Samia Teachers Clinic" kwa ajili ya maslahi ya walimu. Walimu msidanganyike!
- Pre GE2025 - Gulamali: Jimbo letu tumeondoa ziro, sasa hivi tuna one. Asante kwa Rais Samia