Tabora: Mbunge Jacqueline Kainja katika Mapokezi ya Katibu Mkuu UWT Taifa Ndg. Jokate Mwegelo

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

Jacqueline Kainja Andrew, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tabora katika Mapokezi ya Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Taifa, Ndugu Jokate Urban Mwegelo katika Mkoa wa Tabora Wilaya ya Igunga.

Pamoja na mwaliko aliopewa na Kanisa Katoliki kuwa Mgeni Rasmi kwenye Kongamano la Nane la Vijana Wakatoliki Wafanyakazi (VIWAWA) Chama na Jumuiya yake ya Mkoa wa Tabora kilipata nafasi ya kumpokea Katibu Mkuu UWT Taifa, Ndugu Jokate Urban Mwegelo.


"Tunakukaribisha sana Mkoa wetu wa Tabora, Ardhi ya watu wapole na wenye upendo mkubwa. Tunakushukuru kwa Nasaha zako, Hotuba yenye ujumbe mkubwa sana kwa Jamii zetu za Kisukuma na kinyamwezi hasa katika suala la maadili na malezi ili tuweze kuwa na kizazi chenye maadili na utu kwa jamii yetu." - Mhe. Jacqueline Kainja, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tabora.


"Ujio wako katika Mkoa wetu ni baraka na neema kwetu. Karibu sana Tabora kama ambavyo umejionea mapokezi, tunakuahidi hotuba yako tutaifanyia kazi na maelekezo yote uliyotupatia." - Mhe. Jacqueline Kainja, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tabora.


UWT IMARA JESHI LA MAMA
SAMIA USHINDI LAZIMA
SAMIA MITANO TENA
KAZI IENDELEE
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…