Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Wakuu,
Msimamizi mkuu wa uchaguzi wa jimbo la Nzega Vijijini na Bukhene, Mhandisi Modest Apolinary amekanusha kuhusu tuhuma zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zikidai kuwa wakala wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika kituo cha kupigia kura kwenye Chuo cha Ualimu Ndala (TTC) alitolewa na askari katika kituo cha kupiga kura.
Kupata taarifa na matukio ya kimkoa kuhusu Uchaguzi Serikali za Mitaa ingia hapa: LGE2024 - Special Thread: Orodha ya Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari, Mhandisi Apolinary amekanusha kuwa malalamiko hayo sio ya kweli na kwamba askari walifika katika kituo hicho kwa ajili ya kutekeleza majukumu yao ya kusimamia usalama kwenye vituo vya kupiga kura na hawakuingia ndani ya kituo hicho.
Aidha, Apolinary ameeleza kuwa baada ya kusikia malalamiko hayo alifika katika kituo hicho na hakukuta mtu yeyote anayelalamika kuhusu kufukuzwa kwenye kituo hicho.