Tabora: Viongozi wa dini wataka viongozi wapya wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kuwa na hofu ya Mungu na kuwatendea haki wananchi

Tabora: Viongozi wa dini wataka viongozi wapya wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kuwa na hofu ya Mungu na kuwatendea haki wananchi

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Wakuu,

Baadhi ya Viongozi wa dini katika kata ya Kigwa wilaya ya Uyui mkoani TABORA wametaka viongozi wa serikali za vijiji na vitongoji katika kata hiyo waliochakuliwa katika uchaguzi wa Serikali za mitaa mwezi uliopita kutenda haki na kuwa na hofu na Mwenyezi Mungu wakati wakitimiza majukumu ya kuwatumikia wananchi kwenye maeneo yao.

Wakizungumza katika ibada maalum kwa lengo la kuwaombea viongozi hao na kuliombea Taifa amani iliyofanyika katika Kanisa la Sauti ya Mungu Duniani kata ya Kigwa,Askofu wa Kanisa hilo,John Abel Nombo na Sheikh wa Kata ya Kigwa,Said Kadimu wamesema viongozi hao wakiwa na hofu ya Mwenyezi Mungu itasaidia kufanya maamuzi yenye haki kwa wananchi.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa kata ya Kigwa,Emmanuel Fabian aliyemwakilisha mkuu wa wilaya ya Uyui,Mohamed Mtulyakwaku amesema nafasi walizopata viongozi hao ni kwa mpango wa Mwenyezi Mungu hivyo wawaongoze vema wananchi wao na kuendelea kushirikiana na viongozi wa dini.

 
Back
Top Bottom