Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Wajasiriamali wadogo waliopewa eneo la gati la maji nje ya soko la Kachoma, Kata ya Chemchem Manispaa ya Tabora ili wafanyie biashara zao kwa muda huku serikali ikiwatafutia maeneo mapya na sahihi ya kufanyia biashara, wamelalamikia kuvunjwa kwa vibanda vyao usiku wa manane pasi na kutafutiwa maeneo mapya wala kupewa notisi ya kuondoka eneo hilo kisha bidhaa zao zenye thamani ya kuanzia shilingi laki mbili kwenye kila kibanda zikachukulia na wavunjaji ambao bado hawajafahamika.