Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Wakazi wa kata ya Kidongo Chekundu Manispaa ya Tabora wanaoishi karibu na shule ya msingi ya Mpepo wamekubwa na hofu kubwa kwa watoto wao kufa maji pamoja na kubomoka kwa nyumba zao baada mtaro wa maji unaopita pembezoni mwa shule hiyo na makazi yao kuongezeka kina na upana hali inayo inayohatarisha usalama wa wanafunzi na wakazi wa eneo hilo haswa kipindi hiki cha mvua.
baadhi ya wakazi wa eneo hilo Mudathiri Said , Hamis Omary na Sophia Mohamed wameeleza kuwa changamoto hiyo imekuwa ya muda mrefu ambayo mpaka sasa bado haijapata utatuzi.
Aidha, wameeleza kuwa wamekuwa wakitumia muda mwingi kuwafukuza wanafunzi wanaocheza ndani ya mtaro huo ambao unapitisha maji karibu na shule ya msingi ya Mpepo, na kwamba mtaro huo umekuwa ukiongezeka kila siku kuyasogelea makazi ya watu pamoja na shule hali inayowaongezea hofu ya kuwapoteza watoto wao pamoja na makazi yao.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa shule ya msingi ya Mpepo, Shomari Samsekwa ameeleza kuwa mara kadhaa amekuwa akipeleka malalamiko kwenye mamlaka husika juu ya changamoto hiyo pasina mafaniko yoyote, na kubainisha kuwa hali hiyo imesababisha kupungua kwa mahudhurio kwa wanafunzi shuleni kutokana wazazi kuwa zuia watoto wao kutokana na hofu ya kutumbukia kwenye maji.
Kufuatia changamoto hiyo, Jambo TV imemtafuta Mkuu wa WIlaya ya Tabora, Mhandisi Deusdedith Katwale ambapo amesema tayari kuna mkandarasi ambaye amepewa kazi hiyo, na kwamba watawasiliana na Wakala wa Bararbara Mjini na Vijijini (TARURA) kumsimamia mkandarasi huyo ili kutatua changamoto hiyo kwa haraka.