The Palm Beach
JF-Expert Member
- Dec 30, 2015
- 1,967
- 4,267
Sura ya mji wowote hujionesha kwenye maeneo makuu ya kibiashara (business center), soko kuu na stendi kuu ya mabasi...
Kwa wakazi wa Tabora na wasafiri kama mimI mnaofika ktk mji huu wa Tabora mara kwa mara kwa njia ya barabara kwa kutumia usafiri wa bus, mnaweza kuthibitisha hili, kwamba, ukishuka stendi kuu ya mabasi ya mji huu, ukatoka nje kuanza kutembea mtaani mita chache nje ya stendi utakumbana na harufu mbaya kabisa ya kinyesi (maji taka) yanayotiririka hovyo kwenye mifereji ya kawaida ya maji...
Hii si mara ya kwanza au ya pili mimi kufika Tabora na kukumbana na hali ya ajabu kabisa. Ndani ya miezi kama sita mfululizo, nimeshafika Tabora zaidi ya mara nne. Mara ya kwanza, nilifikiri labda ni ajali ya kuzibuka kwa mfereji iliyojitokeza kwa mara moja tu na hivyo ingeshughulikiwa...
Lakini inavyoonekana ndiyo maisha ya kawaida ya wakazi wa mji huu. Leo mimi nimeamua kuwasemea kupitia JF na nina hakika mamlaka husika zitapata ujumbe huu na kuchukua hatua ya kurekebisha haraka sana ili kuokoa afya za watu...
Inashangaza kwamba, mbele ya mifereji isiyofunikwa ya maji tiririka haya machafu ya kinyesi, watu wapowapo tu na wanaendelea na shughuli zao kawaida za biashara ya maduka, chakula, matunda nk kama vile hakuna ubaya wowote...
Hii inaonesha kuwa watu hawa walishaizoea harufu hiyo na kuiona kama hewa ya kawaida tu....
Lakini, I am sure madhara yake ni hawa watu huugua magonjwa ya ajabu lakini wao hudhani labda wanaugua magonjwa ya kawaida tu huku ukweli ukiwa ni magonjwa ya kusababishwa na mamlaka za serikali zisizojali afya za watu wao..
Tunakuuliza wewe Mkurugenzi wa manispaa ya Tabora, Mayor na baraza lako la madiwani na hususani Mamlaka ya Maji Safi na Taka Tabora (TUWASSA) ina maana hamuyaoni mazingira haya machafu na kuchukua hatua haraka za kusafisha? Mnakwama wapi...??