Jerry de Marco
JF-Expert Member
- Aug 16, 2012
- 213
- 41
MARADHI YA KUTOPATA CHOO (CONSTIPATION): Haya ni maradhi ambayo mgonjwa huwa hapati choo kwa wepesi. Haja kubwa inaweza kutoka baada ya siku moja au mbili au zaidi na ikitoka huwa ni kigumu na hutoka kwa shida na wakati mwingine huwa kama
cha mbuzi. Wagonjwa wengine hupata maumivu wakati wa kwenda haja kubwa.
Mtu mwenye afya nzuri hupata haja kubwa kwa kiwango cha chini mara moja kwa siku. Na choo huwa laini na hutoka bila matatizo.
SABABU ZA MARADHI HUSIKA:(1) Upungufu wa vitamini mwilini hasa vitamin B. (2) Maradhi ndani ya utumbo mpana. (3) Kula vitu vigumu na vikavu kama vile vyakula vya ngano. (4) Upungufu wa ulaji matunda na mboga. (5) Kutokunywa maji ya kutosha. (6) Upungufu wa fibre kwenye chakula zinazopatikana kwenye maganda ya mahindi. (7) Ukosefu wa kufanya mazoezi ya viungo.
TIBA: Kanuni ya kwanza:
Chukua glasi moja ya maziwa freshi baridi uchanganye na vijiko viwili vikubwa vya asali na kijiko kimoja kidogo cha mafuta ya habitsoda. Kunywa glasi moja kutwa mara mbili asubuhi na jioni. Dawa hii hufanya choo kuwa laini na kupata haja kubwa kwa wepesi.
Kanuni ya pili: Unga wa sanamaki kijiko kimoja kikubwa, Unga wa tangawizi kijiko kimoja kikubwa, Unga wa habasoda kijiko kimoja kikubwa, na Asali robo lita. Dawa hizi zote zichanganye pamoja kwa kukoroga kwa kijiko. Kula kijiko kimoja kutwa mara tatu.
Kanuni ya tatu: Asali robo lita, na Unga wa Arki susi vijiko vinne vikubwa. Kula vijiko viwili vikubwa kutwa mara mbili.
Kanuni ya nne: Kunywa kwa wingi maji ya kunywa ya kutosha na pia ule kwa wingi matunda na mboga.
Kanuni ya tano: Kula kila siku asubuhi tende saba kabla ya chakula cha asubuhi. Tende hufanya choo kuwa laini. Mkuu.@Jerry de Marco tumia Dawa zangu kisha unipe feedback.
Za jion wana Jf bila mu wazima,tumbo limekuwa likinisumbua dawa nimekunywa lakini shida iliyopo linakuwa linaunguruma kidogo na choo napata kwa shida sana na hapo ni mpaka nijilazimishe lakini kinakuwa si kizuri,wenu ushauri naomben ili niondokane na hii hali
Mkuu Jerry de Marco Nenda Kariakoo Mtaa wa Pemba kawaulize wauza Madawa ya Kiarabu wapemba waliopo karibu na soko kuu la Karişakoo au Mtaa wa Pemba watakupatia mti wa Ark Susi utautwanga utachekecha upate unga wake . tumia kisha unipe Feedback.huo unga wa arki susi ni upi na nitaupataje?
mkuu Bongo Pix Blog Jamaa anaumwa wewe umeamuwa kumpeleka kwenye blog yako?? Umekuja Kutangaza Blog yako hapa kwenye jukwaa la JF Doctor? nenda kule kwenye Jukwaa la Matangazo Madogo Madogo au bonyeza hapa Matangazo madogo Ukatangaze Blog yako hapa tunataka utoe Dawa sio kutangazza mambo ya blog sawa mkuu.Pole sana, tatizo hili lisiposhughurikiwa mapema upelekea kupata saratani ya utumbo mpana COLON CANCER, operesheni ya kuunga utumbo au kifo, Uzuri ni kwamba kuna ufumbuzi tena wa kudumu tafuta uzi waitwa Colon Cancer au TEMBELEA HAPA kwa ufumbuzi zaidi.
Za jion wana Jf bila mu wazima,tumbo limekuwa likinisumbua dawa nimekunywa lakini shida iliyopo linakuwa linaunguruma kidogo na choo napata kwa shida sana na hapo ni mpaka nijilazimishe lakini kinakuwa si kizuri,wenu ushauri naomben ili niondokane na hii hali