Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Rafiki yangu Salum Matimbwa ametukumbusha baba yetu Mzee Kitwana Selemani Kondo. Kanirudisha nyuma mbali sana.
Namkumbuka Kitwana Kondo na Peugeot yake 404 rangi ya kijani ameiegesha pembeni anazungumza Pan Africa, club iliyojitenga na Yanga.
Mzee Kondo hii rangi ya kijani ni kwa kuwa alikuwa mpenzi ya Yanga. Wakati huo sikuwa namfahamu kwa karibu ila kwa kumuona tu.
Alipokuja kunijua alinambia kuwa akimfahamu sana baba yangu na akaniambia kuwa katika ujana wake alipata kupanga nyumba ya mmoja wa bibi zangu Bi. Asha bint Farjallah maarufu akijulikana kama Mama Salehe.
Nyumba hii ilikuwa Mtaa wa Likoma mwisho.
Mama Salehe alikuwa make wa Sheikh Yassin ambae sisi tumezaliwa hakutumkuta alikuwa keshafariki.
Tulichokikuta pale ni madrasa yake ambayo bibi yangu aliiendesha hadi kifo chake na kumbukumbu yangu ya utoto ya madrasa hii ni ile Maulidi ya Mfungo Sita kila mwaka na kipunga chake.
Sisi wajukuu tulikuwa lazima tuhudhurie maulidi ile.
Huyu Salehe ni baba yangu mdogo kwa kuwa mama yake Bi. Asha na mama yake baba yangu Bi. Zena walikuwa ndugu wote mabint Farjallah na alikuwa mtoto pekee wa huyu bibi yangu.
Bwana Salehe akifanya kazi Dar es Salaam Club toka enzi ya ukoloni.
Ninachomkumbuka baba yangu huyu mdogo ni utanashati wake.
Huyu ndiye baba yake Yassin Saleh aliyekuja kuwa golikipa maarufu kufika gadi kucheza Taifa Stars.
Mzee Saleh alikuwa rafiki sana na Mzee Kondo na Dar es Salaam Club ilipofungwa na baba yangu kujikuta hana kazi Mzee Kondo alimpa kazi State Motor Corporation ambako yeye alikuwa Mkurugenzi Mkuu.
Ninapomkumbuka Mzee Kiwana Kondo huja na kumbukumbu za hawa wazee wangu pia na nyakati zao mimi nikiwa mtoto.
Mzee Kondo kaondoka na mengi ndani ya kifua chake.
Lakini kwangu mimi kitu kikubwa alichoniachia kabla ya kufariki kwake ni kunipa jina la kachero wa serikali ya Waingereza aliyekuwa akiwachimba viongozi wa TANU bila ya wao wenyewe kufahamu, taarifa zao zote akiziwasilisha Government House kwa Gavana Edward Francis Twining kwa mdomo.
Sikumuomba Mzee Kondo taarifa hii yeye mwenyewe tu niko nyumbani kwake kwa ajili ya mahojiano ya kipindi cha televisheni aliniita akanimabia nikae pembeni yake ana jambo anataka kuniambia na akaniusia kuwa nisiandike yale atakayonieleza hadi yeye akiwa kesha ondoka duniani.
Mzee Kondo akaniuma sikio na kwa kweli aliyonieleza yalinifungulia kitendawili ambacho kilikuwa kikitaabisha akili yangu kwa miaka mingi kuwa vipi Waingereza waliwafikia Rashid Ali Meli na Iddi Faiz Mafungo kwa urahisi na wakamkamata Iddi Faizi Turiani akitokea Tanga kwa Mwalimu Kihere alipokwenda kuchukua fedha za safari ya kwanza ya Julius Nyerere UNO mwaka wa 1955?
Picha hiyo hapo chini tulipiga siku Mzee Kondo aliponifungulia mlango wa moyo wake kwa upenyo mdogo tu nichungulie ndani.
Mzee Kondo kaingia kaburini na historia kubwa sana ya uhuru wa Tanganyika na mengi mengine.