Tacaids yawahimiza waajiri kuwapima wafanyakazi VVU

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,677

Kila mmoja ana wajibu wa kumlindamwenzake na ugonjwa wa Ukimwi, waajiri tuzingatie kuwapima wafanyakazi VVU

Dar es Salaam. Tume ya Kudhibiti Ukimwi (Tacaids) imewataka waajiri nchini kujenga utaratibu wa kupima afya za wafanyakazi wao mara kwa mara maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) ili kuwa na nguvu kazi imara kwa maslahi ya taifa.

Akizungumza jana wakati wa bonaza la wafanyakazi wa tume hiyo, Mwenyekiti Mtendaji wa Tacaids,Dk Fatma Mrisho alisema kuna haja kwa makampuni, mashirika na waajiri kuweka utaratibu wa kupima afya za wafanyakazi wao mara kwa mara badala ya kusubiri waanguke kwa presha au kufariki ghafla.
Tusiendekeze mikutano na vikao tu na kusahau afya zetu,vita dhidi yaUkimwi inapaswa kupigwa kila kona kuanzia ngazi ya familia, sehemu ya kazi na kwingineko ili taifa lifikie lengo la maambukizi sifuri, vifo sifuri na unyanyapaa sifuri,alisema Dk Mrisho.

Katika bonaza hilo lililobeba kaulimbiu ya ukarimu huanzia nyumbani-pima afya yako wafanyakazi wa tume pamoja na baadhi ya wakazi wa Dar es Salaam waliweza kupata ushauri nasaha nakupima Virusi Vya Ukimwi(VVU) kwa hiari.

Awali Meneja wa Habari wa tume hiyo, Gloria Mziray alisema wamejizatiti kuwa na matukio kama hayo mara kwa mara ili kuhamasisha zaidi upimaji wa VVU mingoni mwa Watanzania.
Kwa mujibu wa ripoti mpya ya utafiti wa viashiria vya VVU na Ukimwi na Malaria Tanzania wa 2011-2012 (THMIS), upimaji wa VVU miongoni mwa wanawake na wanaume ni mkubwa zaidi mijini kuliko vijijini.
Utafiti huo pia unaonyesha kuwa wanawake watatu katika kila wanawake 10 na zaidi ya asilimia 25 ya wanaume wamewahi kupima VVU na kupokea majibu miezi 12 kabla ya utafiti.

Pia ilibainika kwamba, upimaji wa VVU unaongezeka sambamba na ongezeko la kiwango cha elimu kwa wanaume,huku asilimia 54 ya wanaume wenye elimu ya sekondari au zaidi wamepima VVU kupokea majibu ikilinganishwa na asilimia 32 ya wanaume ambao hawana elimu.

© 2013 MCL
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…