elivina shambuni
JF-Expert Member
- May 31, 2018
- 461
- 295
BENKI ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) mpaka sasa imekwisha toa mikopo yenye thamani ya Sh bilioni 141.3 katika miradi mbalimbali ya kilimo, ufugaji na uvuvi. Mikopo hiyo ni sawa na kukopesha asilimia tano ya watanzania wanaojishughulisha na kilimo hapa nchini na zaidi ya asilimia 70 ya watanzania wanajishughulisha na kilimo.
Mkurugenzi wa Utati, Sera na Mipango kutoka benki hiyo, Dk Nyankomo Marwa amesema mikopo iliyotolewa ni kwa ajili ya miradi mbalimbali ya kilimo na kuongeza thamani mazao. Marwa alisema Benki hiyo imejiwekea lengo la kukia zaidi ya asilimia kumi ya wakulima hapa nchini ikapo mwisho wa mwaka huu ili kuboresha kilimo, ufugaji pamoja na shughuli za mnyororo mzima wa thamani wa mazao katika kilimo. “Jumla tuna mikopo ya Sh bilioni 141.3 tangu benki ianze na tumewakia wakulima zaidi ya milioni 1.7 na hawa ni mchanganyiko wa vikundi, mkulima mmoja mmoja na wakulima wadogo, wakati na wakubwa pamoja na viwanda vya uchakataji,” alisema Dk Marwa.
Alisema pia wanaokopeshwa na benki hiyo kupitia vyama mbalimbali vya wakulima pamoja na Vyama vya Msingi vya Ushirika (AMCOS) na viwanda vya uchakataji mazao ili kuwasaidia wakulima wadogo. “Kwa hiyo katika mikopo hiyo pia tunaweza kutoa mkopo kwa kikundi, au kiwanda ambacho kinakopesha wakulima wadogo ili waboreshe kilimo chao na baadae mazao yao kuuza katika kiwanda hicho,” alisema.
Dk Marwa alisema kuwa kwa wakulima wadogo wengi wao hawakopesheki kutokana na masharti ya kibenki, hivyo benki hiyo inawahamasisha kuingia katika vikundi ili kikopeshwe kikundi kuwe na urahisi kuthibiti urudishaji wa mkopo.
Aidha alisema kuwa TADB inashirikiana na benki nyingine pamoja na taasisi za kifedha ambazo ni benki za CRDB, TPB, NMB, Stanbic, Finca, Tandahimba, Mkoba, na Uchumi. “Kwa kupitia benki nyingine washiriki pia tunawakia wakulima na wanapata mikopo huko, tunaamini kwamba sisi hatuwezi kuwa kila mahali yaani kila mkoa na kila Wilaya na vijiji, lakini kupitia hizi benki wakulima tunawakia,” amesema Dk Marwa.