Tafadhali Anne Makinda jihadhari kwani Pius Msekwa si saizi yako. Msekwa katumia usomi kusema akina Halima Mdee wamefutwa Ubunge

Tafadhali Anne Makinda jihadhari kwani Pius Msekwa si saizi yako. Msekwa katumia usomi kusema akina Halima Mdee wamefutwa Ubunge

MdogoWenu

JF-Expert Member
Joined
Dec 23, 2009
Posts
554
Reaction score
916
Mama Anne Makinda,

Nimeona leo mahali unasema vyombo vya habari vimuache Pius Msekwa kwani kalitumikia taifa kwa muda mrefu na sasa ni mstaafu.

Mama Makinda, Pius Msekwa hajastaafu kutumia haki yake ya kutoa maoni kama Katiba inavyomruhusu.

Tatizo siyo Msekwa, tatizo ni wewe hutaki Msekwa aseme kwamba akina Halima Mdee si wabunge tena tangu walipovuliwa uanachama.

Msekwa kanukuu ibara ya 71(1)(e) sasa wewe ulitaka awe kipofu kwa ibara hiyo.

Sasa mama Makinda ngoja nikufundishe mambo matatu inayoelekea huyajui.

Jambo la kwanza ni kwamba Pius Msekwa ndiye mtu pekee aliyebaki hai aliyeshiriki kamati ya kuiunda Katiba hii mwaka 1977.

Kumbuka Mwenyekiti wa kamati hiyo ni alikuwa hayati Thabit Kombo na katibu akawa ni huyu Msekwa.

Wewe ulikuwa wapi wakati huo maana historia haikutaji.

Hivyo Pius Msekwa ni mtunzi wa Katiba yetu bila kujali ni mbovu au nzuri.

Waandishi wanamfuata kwa sababu ni mtungaji wa hiyi Katiba hawakufuati wewe uliyepata uspika kwa kigezo cha Samwel Sitta kukosa jinsia ya Kike mwaka 2010.

Jambo la pili ni kwamba Pius Msekwa ndiye kiongozi pekee ndani ya CCM kuandika vitabu vingi na vinasomwa duniani kote.

Ndiye msomi pekee aliyeandika mengi kuhusu Bunge. Wewe huna article hata ya page moja kwenye gazeti lolote.

Jambo la tatu ni kwamba wiki juzi wakati Bunge hili linazinduliwa Pius Msekwa alialikwa kwenye semina ya wabunge na akatoa lecture nzuri.

Katika semina hiyo Spika Job Ndugai kawaambia kwamba wasiishie kumsikiliza Msekwa kwenye semina ile tu bali wachimbue vitabu vyake vilivyojazana kwenye library ya Bunge.

Jambo la nne ni kwamba kama unataka, japo huwezi, mwambie Pius Msekwa aache kuandika makala zake za "The Current Affairs" kila Alhamsi kwenye gazeti la Daily News.

Serekali inamtumia kila Alhamis kwenye Daily News halafu leo EATV wamemhoji unapiga kelele.

Hivyo kama wewe uliamua kuandika historia ya kukaa kimya basi acha dunia ya wasomi inayomheshimu Msekwa tumheshimu.

Msekwa ndiye mtu pekee ndani ya CCM anayeweza kuongea na wapinzani wakajibizana naye.

Cha muhimu ishauri CCM ipike vijana ma genious kama Nyerere alivyowapika hawa akina Msekwa na siyo hawa wa sasa hivi ambao wakiamka asubuhi wanatafuta tusifie lipi.
 
Mzee Msekwa amewahi sana kutoa tamko lake nazani naye anajua kinachowafukuzwa hao wabunge uanachama wao chadema sio tamko la Mbowe kwenye vyombo vya habari bali ni barua watakazoandikiwa hao watuhumiwa wakielezwa makosa yao na vifungwa na kanuni za chama chao walizovunjwa. Pia Spika wa Bunge kujulishwa rasmi kwa barua.

Sasa kabla ya haya yote kutekelezwa huwezi kusema aliyosema Mzee Msekwa. Tena barua hiya uhakikishe wahusika imewafikia, ambapo na wao wanayo haki ya kuchukua hatua za kimahakama kujitetea.
 
Tatizo ni kwamba leo Msekwa ataonekana mtu wa maana kwa sababu kaongea jambo lenye kuwafurahisha watu fulani ila Msekwa huyohuyo siku nyengine akiongea jambo lisilowafurahisha hata kama ndio ukweli basi ataonekana ni hovyo.

Tuache hii tabia.
 
Hapo ndipo ulipo ujinga wako.
Mkuu hapa ndipo wengi mnapokosea.
Mtu mzima hata kama kakosea kwa maoni yako, bado anastahili lugha ya staha siyo kama hii uliyo tumia hapo juu.

Unapojisifu na kujipa hadhi ya mwanajumuiya ya wasomi basi tumia hekima na busara za kisomi katika mijadala ya kisomi.

Umejenga hoja nyingi nzuri sana kutetea maoni yako lakini lugha hii ya vijiweni imekuangusha sana.
 
Mkuu hapa ndipo wengi mnapokosea.
Mtu mzima hata kama kakosea kwa maoni yako, bado anastahili lugha ya staha siyo kama hii uliyo tumia hapo juu.

Unapojisifu na kujipa hadhi ya mwanajumuiya ya wasomi basi tumia hekima na busara za kisomi katika mijadala ya kisomi.

Umejenga hoja nyingi mzuri sana kutetea maoni yako lakini lugha hii ya vijiweni imekuangusha sana.
Hawa viongozi wastaafu wanatakiwa kuacha kiherehere, wakae kimya kwa sababu ulimwengu wa sasa kila mtu anajua vitu vingi.
 
Na wewe muache Mama Makinda, tatizo lako nini? Unataka uishi maisha yako na pia maisha yake ya kutoa mawazo? Acha ujinga.
 
Back
Top Bottom