Ni kweli kabisa ila hawa watu ninaowazungumzia hawangalii usahihi wanaangalia kama kilichozungumzwa kinaendana na msimamo wao hivyo kinaweza kuwa sahihi ama kisiwe sahihi,na hapo ndio neno "kufarahisha" linapotokea.Kunatofauti Kati ya kufurahisha na kuongea kitu sahihi.
Mh! Hii kali kweli kweli, amekufanya nini huyu mama mpaka unampiga spana nzito namna hii bila huruma?
Na wewe hujasema aliyo yasema mama Makinda .Wewe wa ajabu kweli bilashaka utakuwa kilaza wewe hivi umesoma na kuelewa vizuri maoni ya Mama Makinda? Hoja yako haina mashiko umekurupuka usimlishe mama Makinda maneno yako.
Kwani lazima aongee msekwa tu, mbona katiba ipo wazi Sana labda uamue kukaza fuvu kama Wenzio WA lumumbaTatizo ni kwamba leo Msekwa ataonekana mtu wa maana kwa sababu kaongea jambo lenye kuwafurahisha watu fulani ila Msekwa huyohuyo siku nyengine akiongea jambo lisilowafurahisha hata kama ndio ukweli basi ataonekana ni hovyo.
Tuache hii tabia.
Nadhani hujaelewa mkuu.Kwani lazima aongee msekwa tu, mbona katiba ipo wazi Sana labda uamue kukaza fuvu kama Wenzio WA lumumba
Pascal Njaa Yuko kwake anajililia machozi baada ya Chakubanga Polepole kuteuliwa na yeye hajateuliwa .Hapa Pascal Mayalla na johnthebaptist nawasubiri watoe ya moyoni
Tuwekee rejea, usituwee hisia zako. Mzee Msekwa amejibu kulingana na alivyoulizwa na mwandishi na akarejea Katiba ya nchi. Kama umemsikiliza vizuri yeye wala hakujikita kwenye ule uhuni uliofanywa na NEC pamoja na mzee Ndugai. Yeye amejibu kana kwamba wale Covid-19 walikuwa "wabunge halali" ila madam chama kimewatema, basi Ndugai asijiingize kabisa kwenye jambo hilo.Mzee Msekwa amewahi sana kutoa tamko lake nazani naye anajua kinachowafukuzwa hao wabunge uanachama wao chadema sio tamko la Mbowe kwenye vyombo vya habari bali ni barua watakazoandikiwa hao watuhumiwa wakielezwa makosa yao na vifungwa na kanuni za chama chao walizovunjwa. Pia Spika wa Bunge kujulishwa rasmi kwa barua.
Sasa kabla ya haya yote kutekelezwa huwezi kusema aliyosema Mzee Msekwa. Tena barua hiya uhakikishe wahusika imewafikia, ambapo na wao wanayo haki ya kuchukua hatua za kimahakama kujitetea.
Mkuu hapa ndipo wengi mnapokosea.
Mtu mzima hata kama kakosea kwa maoni yako, bado anastahili lugha ya staha siyo kama hii uliyo tumia hapo juu.
Unapojisifu na kujipa hadhi ya mwanajumuiya ya wasomi basi tumia hekima na busara za kisomi katika mijadala ya kisomi.
Umejenga hoja nyingi nzuri sana kutetea maoni yako lakini lugha hii ya vijiweni imekuangusha sana.
Uongo au makosa ya mkubwa yana maana zaidi kuliko ukweli au usahihi wa mdogo.
The Boss is always right.
Kwa mantiki hii Mama Makinda anaweza kukosolewa na mtu wa haiba yake au zaidi ikaleta maana.
Aliyeleta mada hii tunaomba CV yake tafadhali vinginevyo hakuna sababu ya kuchangia.
Mimi nafikiri kwa akili iliyosahihi, ikitokea Mzee Msekwa, mtu au kiongozi yeyote yule akatoa mawazo yake kwenye Jambo lolote ambalo linathibitika kuwa kinyume na ushauri aliotoa, kumkosoa ni halali, lakini kwa hili la wabunge was chadema Mzee Msekwa ameongea kwa reference ya katiba Kama ilivyo Sasa, utamkosoa kwa kutumia reference ipi?
mzee hajakosolewa yeye binafsi na makinda,makinda anasema na wanahabari.
mimi nasema na mleta mada kumkosoa ane makinda.
Soma vizuri uelewa kwanzMsekwa ndio aliitengeneza katiba ya JMT ya mwaka 1977!
Wewe sio mdogo wetu Bali mkubwa wetu.!! Hongera sana mkuu .viongozi wengi wana jibu hoja kulinda matumbo yao haijalishi wanajua ukweli. I salute you man!!Mama Anne Makinda,
Nimeona leo mahali unasema vyombo vya habari vimuache Pius Msekwa kwani kalitumikia taifa kwa muda mrefu na sasa ni mstaafu.
Mama Makinda, Pius Msekwa hajastaafu kutumia haki yake ya kutoa maoni kama Katiba inavyomruhusu.
Tatizo siyo Msekwa, tatizo ni wewe hutaki Msekwa aseme kwamba akina Halima Mdee si wabunge tena tangu walipovuliwa uanachama.
Msekwa kanukuu ibara ya 71(1)(e) sasa wewe ulitaka awe kipofu kwa ibara hiyo.
Sasa mama Makinda ngoja nikufundishe mambo matatu inayoelekea huyajui.
Jambo la kwanza ni kwamba Pius Msekwa ndiye mtu pekee aliyebaki hai aliyeshiriki kamati ya kuiunda Katiba hii mwaka 1977.
Kumbuka Mwenyekiti wa kamati hiyo ni alikuwa hayati Thabit Kombo na katibu akawa ni huyu Msekwa.
Wewe ulikuwa wapi wakati huo maana historia haikutaji.
Hivyo Pius Msekwa ni mtunzi wa Katiba yetu bila kujali ni mbovu au nzuri.
Waandishi wanamfuata kwa sababu ni mtungaji wa hiyi Katiba hawakufuati wewe uliyepata uspika kwa kigezo cha Samwel Sitta kukosa jinsia ya Kike mwaka 2010.
Jambo la pili ni kwamba Pius Msekwa ndiye kiongozi pekee ndani ya CCM kuandika vitabu vingi na vinasomwa duniani kote.
Ndiye msomi pekee aliyeandika mengi kuhusu Bunge. Wewe huna article hata ya page moja kwenye gazeti lolote.
Jambo la tatu ni kwamba wiki juzi wakati Bunge hili linazinduliwa Pius Msekwa alialikwa kwenye semina ya wabunge na akatoa lecture nzuri.
Katika semina hiyo Spika Job Ndugai kawaambia kwamba wasiishie kumsikiliza Msekwa kwenye semina ile tu bali wachimbue vitabu vyake vilivyojazana kwenye library ya Bunge.
Jambo la nne ni kwamba kama unataka, japo huwezi, mwambie Pius Msekwa aache kuandika makala zake za "The Current Affairs" kila Alhamsi kwenye gazeti la Daily News.
Serekali inamtumia kila Alhamis kwenye Daily News halafu leo EATV wamemhoji unapiga kelele.
Hivyo kama wewe uliamua kuandika historia ya kukaa kimya basi acha dunia ya wasomi inayomheshimu Msekwa tumheshimu.
Msekwa ndiye mtu pekee ndani ya CCM anayeweza kuongea na wapinzani wakajibizana naye.
Cha muhimu ishauri CCM ipike vijana ma genious kama Nyerere alivyowapika hawa akina Msekwa na siyo hawa wa sasa hivi ambao wakiamka asubuhi wanatafuta tusifie lipi.
Ndiyo nimemkosoa Anne Makinda