Tafadhali Ewe Mwanaume uliyemtesa Mtangazaji wa Magic fm Mary Edward mwombe radhi utuokoe Wanaume wote!

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Ni Mtangazaji ambaye ukiwa unamsikiliza akitangaza au hata akiwa anachangia mada fulani katika Kipindi chao cha asubuhi hutopata shida sana kujua ya kwamba lazima tu alikuwa na Mahusiano mabaya huko nyuma na Mtu wake na alimtenda vibaya mno ndiyo maana huwa anakuwa ' very emotional ' kwa mambo ya Kimahusiano yanayowahusu Wanaume.

Mary Edward Mzurikwao hajawahi kuwa ' neutral ' katika ' udadavuaji ' wake wa masuala ya Kijinsia au Mahusiano na kuna muda utaona kabisa kwamba tukio fulani limemtokea Mwanamke mwenzake kwa Kosa lake mwenyewe lakini bado utamsikia Mtangazaji huyu akiendelea kuwaponda / kuwananga / kuwasema Wanaume utadhani labda Mimba iliyomleta Yeye hapa duniani haikutokana na juhudi za huyo huyo Mwanaume ambaye leo anamchukia.

Mtangazaji Mary Edward amekuwa na tabia za kulazimisha mambo ambayo hata Kidini tu na Kimaadili ya Kiafrika hayawezekani kiasi kwamba huwa namtafakari na simpatii majibu sana sana huwa naona ananikera tu.

Kwa mfano leo asubuhi amekazania kabisa kusema tena kwa amri kabisa akitutaka Wanaume wote kuwa na tabia za kuwauliza Mabinti zetu kama wapo katika Siku zao za Hedhi ( Menstrual Period / Cycle ) na kisha tuwe tunaenda kuwanunulia Madukani na kuwapa ili wazitumie na kwamba ikiwezekana tuwe pia tunawauliza kama wamemaliza Siku zao na kuwafundisha jinsi ya Kuoga ili ' Kujiswafi ' vizuri huko ' Ikuluni ' Kwao.

Hivi huyu Mtangazaji Mary Edward na Yeye Baba yake Mzazi alikuwa akimfanyia yote haya pale alipovunja Ungo? Halafu ni kwanini anapenda sana kuitumia Magic fm kama ' platform ' yake ya kuwasema vibaya Wanaume? Kama aliumizwa na kuudhiwa na Mahusiano yake na Mwanaume wake tafadhali watafutane kimya kimya na wayamalize lakini siyo kila uchao kujifanya anakuwa ' too emotional ' kwa ' issues ' za Wanaume.

Abadilike upesi tafadhali na naamini kwa ' Uzi ' wangu huu ' message sent and delivered ' na Kesho kama kawaida yangu nitakisikiliza Kipindi chao ili nione ' reaction ' yake juu ya huu ' Uzi ' hasa nikiamini kwamba karibia 99% ya Watangazaji wa hicho Kipindi ni wana JF wazuri tu na tunao humu 24/7 tukitiririka na kuserereka pamoja.

Nawasilisha.
 
Ila nawewe ume panic ,,labda ndiye uliye sababisha huyu bint achukie vijana wetu.

Hapana Mkuu nimeanza kumfuatilia huyu Binti na aina yake hii ya Utangazaji muda mrefu sana na huko nyuma nilidhani labda angebadilika au hata Wenzie ' Kipindini ' wakiongozwa na ' Program Chief Host ' wao Orest Kawau, Salum Mkambala na Kibwana Dachi lakini kumbe hadi leo bado ameendelea nayo hii tabia na ndiyo maana nikiwa kama Mwanaume uvumilivu Kwake juu ya hili umenishinda na nimeamua ' Kumchana ' mubashara kabisa. Na kama kawaida yangu sijawahi ' Kumchamba ' Mtangazaji humu kwa ' mapungufu ' yake na asibadilike hivyo naamini kupitia ' Uzi ' huu huyu Mtangazaji Mary Edward Mzurikwao nae atabadilika kwani ukiachilia mbali hili ' pungufu ' lake moja ila ni Mtangazaji mzuri sana na ana Sauti si tu nzuri mno ya Kumsikiliza bali ni tamu sana masikioni mwa msikilizaji.
 
daahhh" huyo demu akili hana "" Nina muda mrefu sasa tangu niache kuisikiliza hiyo radio ""....lakini niliwahi kuisikiliza mwaka jana kama sijasahau ..na huyo demu alikuwa anaongea ongea ujinga wake huo huo unaousema"" eti baba anatakiwa kuwa anamnunulia mwanae wakike chupi ..brazia..na pedi ""..daahh nilisstaajabu sana kwakweli""....
 
Leo Asubuhi mida ya saa tatu waliondolewa studio watangazaji wote na producer wao wa kipindi cha mseto.

Sijaelewa walikuwa na kosa gani, mwenye taarifa zaidi azitoe, maana nilifungulia hiyo station nikakuta bosi wao anafoka na kuwasuspend warudi nyumbani.
Akaomba radhi kwa wasikilizaji, zikaendelea kupigwa ngoma tu hadi saa nne.

Mwenye kujua kosa lao aliweke bayana tufahamu.
 

Bosi wao Mkuu Dada yangu Madam Dina Chahali ( kama bado hajahama hapo AMG ) nina uhakika tupo nae hivyo anaweza kutusaidia na kutupa ushirikiano juu ya hili. Na kama hawezi basi ' Mabrazameni ' akina Nicky Ngonyani na mwenzake Dativas Mango ambao nao pia ni sehemu ya ' Management ' hapo wanaweza kutusaidia kutupa ufafanuzi Kuntu katika hili.
 
GENTAMYCINE hata wewe kuna mwanamke ulimuumiza sana na Bado hujamuomba msamaha.

Mimi mademu zangu wote huwa namalizana nao pale pale kama Kondakta na Abiria ndani ya Daladala sasa leo unavyoniambia kuna Demu sijui nilimkosea na sijamwomba Msamaha nashindwa Kukuelewa! Niliacha kupenda rasmi, kuwanyenyekea hawa Viumbe na Kuwabembeleza kama Mwendawazimu mwaka 2010 na sasa hivi ukinikuta namwambia Demu ' Nakupenda ' jua namjaza tu Upepo / namtengeneza anipanulie ' Kitufe ' chake Mwanamume nipite zangu na nionyeshe ' Urijali ' wangu uliotukuka Kwake kisha ndiyo ' ntolee ' hiyo.
 
Nimemsikia Leo asubuhi yan sikumuelewa kabisa
 
Kama yupo humu hili dongo litakua limempata la uso[emoji3]
Ngoja tuangalie replies za waliopanic tumfume[emoji23]
 
Hapo kwenye bold usipo fanya ufafanuzi then mi nita conclude kwamba hata wewe uliumizwa na demu mwaka hu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…