VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,137
- 17,908
Kama Tume yako imeandaa Rasimu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wenye kujumuisha zilizokuwa nchi huru,tena Jamhuri, za Tanganyika na Zanzibar,iweje sisi tuitwe Tanzania Bara na wenzetu wabakie kuwa Zanzibar? Sisi watanganyika tutaandika Katiba yetu. Katiba itakuwa na jina la nchi yetu. Tunaweza kujiita tutakavyo. Wengi wetu twapenda tuitwe tena Tanganyika. Na tutaandika Katiba ya Tanganyika wala si ya Tanzania Bara.Subirini tuanze mchakato. Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam