VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,137
- 17,908
Kama Tume yako imeandaa Rasimu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wenye kujumuisha zilizokuwa nchi huru,tena Jamhuri, za Tanganyika na Zanzibar,iweje sisi tuitwe Tanzania Bara na wenzetu wabakie kuwa Zanzibar? Sisi watanganyika tutaandika Katiba yetu. Katiba itakuwa na jina la nchi yetu. Tunaweza kujiita tutakavyo. Wengi wetu twapenda tuitwe tena Tanganyika. Na tutaandika Katiba ya Tanganyika wala si ya Tanzania Bara.Subirini tuanze mchakato. Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
Wewe Mkuu ndiye unayepotosha.Ima kwa kutoelewa kilichoandikwa au kwa makusudi.Tanganyika imetajwa kwenye Utangulizi tu. Haikutajwa kwenye Ibara yoyote ya Rasimu. Nakuonjesha Ibara Ndogo ya 2 ya Ibara ya 146 ya Rasimu kuhusu Mahakama Kuu.Inasema hivi:(2)Mahakama Kuu ya Tanzania Bara na Mahakama Kuu yaHivi wakuu hii rasimu mmeisoma yote au mmekimbilia huku mitandaoni na kuanza kupiga kelele za bure? Kama mmesoma msingeweza kuandika hiki mlichokiandika. Rasimu imetamka wazi wazi uwepo wa Tanganyika na Zanzibar kuanzia ukurasa wa 76. In fact, ukarasa huo ni SURA YA NANE inayohusu VYOMBO VYA DOLA VYA TANGANYIKA NA ZANZIBAR. Sehemu ya kwanza inahusu serikali ya Tanganyika na Zanzibar, sehemu ya pili mabaraza ya Wawakilishi ya Tanganyika na Zanzibar (page 77), sehemu ya tatu mahakama kuu za Tanganyika na Zanzibar (page 78). Sasa huu upotoshaji sijui nyie wenzangu mmeutoa kwenye rasimu ipi?
Mkuu sorry, nilikuwa na draft tofauti. Kuna draft mbili ambazo zina tofauti kubwa, wengi tunaweza ingia kwenye njia panda hiiWewe Mkuu ndiye unayepotosha.Ima kwa kutoelewa kilichoandikwa au kwa makusudi.Tanganyika imetajwa kwenye Utangulizi tu. Haikutajwa kwenye Ibara yoyote ya Rasimu. Nakuonjesha Ibara Ndogo ya 2 ya Ibara ya 146 ya Rasimu kuhusu Mahakama Kuu.Inasema hivi:(2)Mahakama Kuu ya Tanzania Bara na Mahakama Kuu ya
Zanzibar zitakuwa na mamlaka sawa ya kusikiliza katika ngazi ya awali,
mashauri ya madai na jinai kuhusu Mambo ya Muungano katika maeneo
ya utawala ya Washirika wa Muungano.